Katika kikao hicho ambacho kimefanyika Leo hii Katika Ukumbi Mkubwa wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza kikiongozwa na Mwenyekiti Mhe.Amina Makilagi ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana amesema Bajeti ya fedha ndani ya Wilaya ya Nyamagana kwa Mwaka 2026/2027 itafanya mabadiliko mbalimbali ndani ya Wilaya ikiwemo juu ya ujenzi wa miundombinu kama Barabara na Huduma za Kijamii ( Mashule,vituo vya afya n.k)
Ndani ya Bajeti ya fedha 2026/2027 ambayo imekusanya ajenda kama Bima ya Afya kwa wote,Mapendekezo ya Mpango wa Bajeti ya Matumizi na Mapato lakini Pia Makadilio ya Makusanyo yatokanayo na ruzuku kutoka Serikali Kuu ajenda zote hizi zitajadiliwa na Madiwani wa Kata mbalimbali za Wilaya ya Nyamagana kabla ya kupitishwa na kuwasilishwa ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Aidha ; Katika Bajeti hii itafanya Tathimini Juu ya Ujenzi wa Masoko Makubwa ndani ya Wilaya ya Nyamagana ambayo yatawakutanisha wafanyabiashara mbalimbali kwa pamoja na changamoto ya watu kufanya biashara kando ya Barabara kutatulika.
Mhe.Amina Makilagi amesisitiza suala la amani pia kwa wananchi wote wa Wilaya ya Nyamagana bila ya kubaguana Katika Imani za Kidini na Kikabila.
"Amani ndio Kila kitu,Tusibaguane Kidini wala Kikabila Amani ni Msingi wa Kila kitu"
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.