Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi yafurahishwa kwa namna Halmashauri inavyotekeleza miradi ya Ujenzi wa Madarasa na Vyoo kwa Ufanisi
Kamati ya siasa ya Chama Tawala imefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa mwaka wa fedha 2017/2018. Miradi iliyokaguliwa ni pamoja na Ujenzi wa madarasa shule ya Msingi Nyangulugulu,Ujenzi wa Matundu ya Choo Mahina Sekondari , Kituo cha Afya Igoma , Machinjio ya Kisasa –Mhandu, Ujenzi na Ukarabati wa madarasa Igoma C, Ujenzi wa Vyoo Kishiri shule ya Msingi, na Ujenzi wa Madarasa Fumagila.
Kamati ya siasa ikiwa shule ya Msingi Kishiri walikoshwa kwa namna Uongozi wa kata unavyoshirikiana na Viongozi wa Mitaa na Ungozi wa shule kutekeleza maendeleo “ Tumefurahishwa sana kwa namna mnavyofanya kazi kwa uwazi na ushirikiano mkubwa mmesema mlipewa Fedha kwa ajili ya Matundu tisa tu ya choo lakini mkajenga kumi na moja kwa kweli huu ndio uzalendo unaohitajika ‘’alisema Mwenyekiti wa Chama wilaya
Aidha kwa utendaji huo uliotukuka Kamati ya siasa ya wilaya iliagiza Mkurugenzi Kumpandisha cheo Kaimu Mtendaji wa Kata ya Kishili Ndugu John Mwakilasi kuwa Mtendaji wa Kata .Akizungumza Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Ndugu Kiomoni Kibamba alihaidi kujenga madarasa mengine mawili kwenye hiyo shule na kuongeza walimu wanane kwa ajili ya kutimiza Ikama
sehemu ya kusafishishia mikono na nyama kwenye machinjio ya kisasa - Mhandu
Muonekano wa choo kilichojengwa Shule ya Msingi Kishili
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.