Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Mwanza Ndg. Michael Lushinge Masanja Leo Mei 27, 2024 ameiongoza kamati hiyo kukagua Miradi mitano ya Maendeleo ya kimkakati yenye thamani ya Bilioni 66 inayotekelezwa na Halmashauri ya Jiji la Mwanza na Taasisi Nyingine mbalimbali Jijini Mwanza Chini ya uongozi wa Serikali ya awamu ya sita Inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Ukaguzi huu wa Miradi ya Maendeleo umefanywa ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Miradi ambayo imekaguliwa ni pamoja na Mradi wa ujenzi wa Soko Kuu la Kisasa lililopo mjini Kati ambalo limefikia asilimia 95, Mradi wa Gati la maegesho ya Meli ya Mv. Mwanza Hapa kazi tu,uliopo eneo la Mwanza Kasikazini. Miradi mingine ni Chanzo cha Maji kilichopo Kata ya Butimba ambao umekamilika kwa asilimia 100, ujenzi na uboreshaji wa Zahanati kuwa Kituo Cha Afya Mkolani ambao umekamilika kwa asilimia 100 na ujenzi wa mradi wa Barabara ya Buhongwa - Igoma ambao umefikia asilimia 30.
Akizungumzia mradi wa Barabara ya Buhongwa- Igoma Ndg. Michael Masanja amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe, Said Mtanda kuhakikisha anausimamia mradi huo kwa ufasaha Ili uweze kukamilika kwa wakati na kuanza kazi mara moja ikiwa ni sambamba na kumtaka Mhe. Mtanda kushughulikia utatuzi wa mvutano uliopo kwa watu wa TANESCO na Idara ya maji kuhusu kutoa mitambo yao katika eneo ambalo barabara inajengwa ili kuharakisha ujenzi wa barabara kukamilika kwa wakati.
Mwisho Ndg. Michael amehitimisha kwa kuutaka uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, kutenda haki pindi tu ujenzi wa soko hilo utakapokamilika kwa kuwapa kipaumbele wale wote waliokuwa wakifanya biashara eneo hilo hapo awali.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.