Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Mwanza limeandika historia ya kuwa Baraza la kwanza kulitembelea Jiji la Dodoma baada ya kupandishwa hadhi hiyo Aprili, 26, 2018.Lengo kuu la ziara ikiwa ni kubadilishana uzoefu hususan katika suala la usafi na Mazingira
Katika ziara hiyo waheshimiwa madiwani wakiongozwa na Naibu meya wa Jiji la Mwanza Mheshimiwa Bhiku Kotecha wamepata fursa ya kulitembelea Dampo la kisasa la kuhifadhia taka kwa njia ya kuzifukia chini (Sanitary land fill) lilopo eneo la Chidaya kata ya Matumbulu nje kidogo ya Jiji Dodoma.
Wakiwa katika Dampo hilo walipata maelezo ya kina juu ya mradi huo kutoka kwa Mhandisi wa Mazingira wa Jiji la Dodoma Barnabas Faida, ambaye aliwaeleza kuwa mradi huo umegharimu Bilioni 7.1 na umetumia zaidi ya Hekari 48 ambapo kwa siku linachukua tani 120 hadi 140 za taka Mradi huo ulianza kutekelezwa tangu 2011 kwa fedha za serekali ikiwa ni mkopo kutoka Benki ya Dunia kupitia mradi wa kuimarisha Majiji ya kimkakati (TCSP)
Aidha waheshimiwa madiwani pamoja na wataalamu waliombatana nao walipata fursa ya kulitembelea Bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania wakiongozwa na Mwenyeji wao Mheshimiwa Stanslaus Mabula Mbunge wa Nyamagana
Katika ziara hiyo Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Ndugu Godfrey Kunambi alifurahia ujio wa ugeni kutoka halmashauri ya jiji la Mwanza na kuomba uhusiano huo kuendelea kudumu maana “kupitia mahusiano haya tutabadilishana uzoefu maana ninyi wenzetu mnauzoefu wa kutosha ya namna ya kuliendesha Jiji hivyo kupitia mahusiano haya tutajifunza kwenu” alisema Ndugu Kunambi.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.