Taasisi ya SUKOS KOVA Tanzania na Vodacom Tanzania wametoa vifaa vya uokoaji kama vile Vifaa vya kuzimia moto,Vifaa vya kuogelea vyenye thamani ya Shilingi Milioni 120 wilayani Nyamagana,wanufaika wakiwa Jeshi la Zima moto, Wavuvi Shule ya Msingi Nyamagana, Sweya na Luchelele
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo Mkuuu wa wilaya ya Nyamagana Dkt Phillis Nyimbi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella amewashukuru wadhamini wa vifaa hivyo kwa nia yao njema ya kusaidia watu wa kanda ya ziwa kuweza kujiokoa na majanga mbali mbali yanayoweza kujitokeza
"Nimshukuru Mkurugenzi wa SUKOS KOVA na Vodacom Tanzania kwa nia yao njema ya kuwasaidia wana Mwanza.Hivi vifaa vikitumiwa ilivyokusudiwa itasaidia kupunguza na kutuepusha na baadhi ya majanga" amesema Dr Nyimbi
Aidha Dr Nyimbi amewataka watu wote waliopata vifaa hivyo vikatunzwe vyema na kutumika kwa maslai ya wengi na sio watu binafsi .
Akiongea kwa niaba ya Taasisi ya SUKOS KOVA foundation, Kamishna mstaafu wa Jeshi la Polisi Suleman Kova amesema ameguswa na kuona ni vyema Taasisi yake kujikita kutoa Elimu na vifaa kwa watanzania namna ya kujikinga na kujiokoa na majanga mbali mbali yanayotokea kwenye jamii zetu.
Hata hivyo Ndg Kova amewataka wadau wengine kuiga mfano wa Vodacom Tanzania na kuchangia vifaa mbali mbali kwa ajili ya kusaidia uokoaji wakati wa majanga,
Akitoa salam za Halmashauri ya Jiji la Mwanza Naibu Meya wa Jiji la Mwanza Mhe Bhiku kotecha amewashukuru wadau hao wa maendeleo kwa kulichagua Jiji la Mwanza na hususan Kata ya Nyamagana kuwa sehemu ya uzinduzi wa programu hiyo.
Pamoja na hilo, Mhe Kotecha amesema ataendelea kuwa balozi mzuri wa Vodacom Tanzania kutokana na Vodacom kutoa mchango mkubwa mara kwa mara kusaidia jamii.
Naibu meya ameendelea kuwaomba Vodacom Tanzania kuja kuwekeza kwenye uwanja wa kisasa wa mpira wa miguu wilayani Nyamagana kwa kujenga majukwaa ya kukaa watu nao pia watapata fursa ya kutangaza matangazo yao ya biashara.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.