Kamati ya siasa mkoa wa Mwanza yafanya ziara na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri ya Jiji la Mwanza yenye thamani ya jumla ya TSHs 17,568,356,560/=
Ikikagua miradi ya maendeleo Kamati hiyo, iliyoongozwa na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa (NEC) Ndg; Jamal Babu amepongeza jitihada zinazofanywa na uongozi mzima wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa kuwaletea wananchi maendeleo katika sekta zote ikiwamo Elimu, Afya, Maji, Viwanda na Miundombinu ya Barabara ambayo serikali hii ya awamu ya tano inasisitiza zaidi.
Ndg; Jamal pia amempongeza Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Ndg Kiomoni Kibamba kwa ubunifu mkubwa wa kuanzisha kiwanda cha matofari kilichopo Buhongwa (Dampo), kiwanda ambacho kinafyatua matofari na kuyapeleka kwenye Kata mbalimbali za Jiji la Mwanza kwa ajili ya ujenzi wa madarasa, vituo vya afya na miradi mingine ya maendeleo ambayo tayari wananchi wameanzisha ujenzi wake kwa kujenga misingi.
Kamati pia imesisitiza na kushauri Halmashauri zingine za Mkoa wa Mwanza kujifunza kutoka Halmashuri ya Jiji la Mwanza kwani, serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Raisi John Pombe Joseph Magufuli inawataka watanzania wote kufanya kazi na kuwa wabunifu ili kuleta maendeleo haraka kama kauli mbiu yake isemavyo “Hapa Kazi tu” kauli ambayo inatekelezwa kwa vitendo na Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa miradi inayoajiri wananchi na pia kusogeza huduma muhimu kwa wananchi wake.
Akihitimisha ziara hiyo Ndg Jamal amesema ni lazima Chama cha Mapinduzi kupitia Kamati zake za siasa ngazi zote kufanya kazi kwa pamoja na serikali ili kuleta maendeleo kwa wananchi waliokiamini na kukipa chama hicho ridhaa ya kuwaongoza. Alisema, yanayotekelezwa na serikali ni yale ambayo CCM kupitia wagombea wake iliyaahidi kwenye ilani ya Uchaguzi ya 2015-2020.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na mradi wa ujenzi wa soko la mlango mmoja TSHs 72,838,750, upanuzi wa kituo cha Afya Igoma TSHs 400,000,000/=, ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa mawili na Ukamilishaji wa matundu 25 ya vyoo Shule ya Sekondari Buhongwa TSHs 46,000,000/=, ujenzi wa dampo la kisasa Buhongwa na barabara za rami 3.12 KM Mwanza Mjini TSHs 15,912,434,395/=, ujenzi wa kiwanda cha kufyatua matofali Buhongwa TSHs 98,191,000, mradi wa kuboresha maji safi na mazingira, ujenzi wa barabara ya mawe Nyamazobe 888,292,415 na ujenzi wa Zahanati ya Kata Mkuyuni TSHs 150,000,000/=.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.