Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe; Selemani Jafo ameisifu Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa kasi na viwango vya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Waziri Jafo ameyasema hayo alipofanya ziara ya kustukiza wakati alipokagua utekelezaji wa ujenzi wa madarasa matano maarufu kama "madarasa ya Magufuli" katika shule ya Msingi Iseni iliyoko Kata ya Butimba Jijini Mwanza.
Akizungumza na viongozi na wananchi waliokuwepo katika ukaguzi huo Waziri Jafo alishangazwa na spidi ya utekelezaji na pia kiwango cha thamani ya fedha katika utekelezaji wa mradi huo wa madarasa. "Mhe; Rais Magufuli alitoa agizo la ujenzi huu tarehe 08 Disemba2019 na leo tarehe 03 January 2020 mradi umefikia hatua ya kuezeka? na tena mmetumia milioni 29 tu, fedha za ndani! Kwa kweli mnastahili pongezi na Halmashauri zingine nchini ziige mfano huu" alisema Waziri Jafo.
Pamoja na kutoa sifa hiyo kwa mradi wa madarasa, Waziri Jafo alisema amewahi kukagua miradi ya Afya (Kituo cha Afya Igoma), elimu (Nganza Sekkndari), ujenzi wa miundombinu ya barabara (Nyamazobe) na mingine mingi na mara zote amekuwa akiridhishwa na kiwango cha utekelezaji na thamani ya fedha.
Ziara hii ilitokana na Waziri Jafo kuhudhuria Tamasha la Utoaji tuzo kwa walimu, wanafunzi, shule na kuwaaga wastaafu wote wa elimu msingi kuanzia Januari hadi Disemba 2019 lililofanyika viwanja vya CCM Kirumba tarehe 03 Disemba 2020.
Akizungumza na walimu na watumishi wengine waliohudhuria tamasha hilo, Waziri Jafo alitoa maagizo kwa maafisa Utumishi wa Halmashauri zote nchini kuzingatia utoaji wa stahiki za watumishi ikiwa ni Pamoja na kulipa malimbikizo na kuwapandisha madaraja watumishi wanaostahili.
Alisema maafisa Utumishi wanaojifanya miungu watu sasa wakati wao umekwisha.
Tamasha la utoaji wa tuzo liliambatana na michezo mbalimbali ikiwamo mpira wa miguu, mpira wa wavu, netball, kuvuta kamba na utoaji wa zawadi kwa walimu, shule, Kata,na wanafunzi waliofanya vizuri katika matokeo ya darasa la saba mwaka 2019.
Halmashauri ya Jiji la Mwanza ilikuwa ya nne kitaifa katika matokeo ya elimu msingi 2019 na inalenga kuwa ya kwanza kitaifa.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.