Halmashauri ya Jiji la Mwanza inatarajia kukusanya jumla ya shilingi bilioni 22 katika bajeti ya mwaka wa fedha 2022/ 2023.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Ndg; Sekiete S, Yahaya alipokuwa akikabidhi madarasa 39 yaliyojengwa na fedha za mpango wa maendeleo kwa ustawi wa taifa,mapambano dhidi ya UVIKO 19.
Akikabidhiwa madarasa hayo,Katibu tawala wa Mkoa wa Mwanza Ndg; Ngusa Samike amepongeza makisio hayo ya bajeti na kuipongeza Halmashauri kwa kukusanya zaidi ya bilioni11 hadi kufikia nusu ya mwaka wa bajeti ikiwa ni sawa na asilimia 53 ya makusanyo ya mwaka wa fedha 2021/2022.
Sherehe za makabidhiano ya madarasa 39 zimefanyika leo tarehe 04 Januari, 2022 na kuhutimishwa katika viwanja vya shule ya sekondari ya Luchelele ikihudhuriwa na waheshimiwa madiwani,viongozi wa Chama Cha Mapinduzi,watendaji wa serikali na wananchi.
Katika sherehe hizi,kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel,RAS ameipongeza Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa kutekeleza mpango huu kwa kujenga madarasa ya ghorofa kwakuwa utaratibu huu unazingatia matumizi bora ya ardhi.
Ameipongeza pia serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa maamuzi yake ya kuupatia Mkoa wa Mwanza jumla ya shilingi bilioni 20.5 itakayojenga madarasa 1017 hasa ikizingatiwa uhitaji mkubwa wa vyumba hivyo kwa wakati huu wa usajili wa watoto wa kidato cha kwanza.
Akitoa shukrani zake, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mhe; Amina Makilagi ameipongeza serikali ya awamu ya sita,Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na kushukuru ushirikiano alioupata kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji,ofisi ya Mbunge wa Nyamagana,wadaau na wananchi wote katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuomba ushirikiano uendelee ili Nyamagana iwe ya mfano.
Halmashauri ya Jiji la Mwanza imepokea jumla ya shilingi bilioni 1.96 na kujenga madarasa 39 ya chini kwa gharama ya shilingi milioni 780 na shilingi bilioni 1.9 inatumika kujenga ghorofa 13 zenye vyumba 64 vya madarasa ambayo yatakabidhiwa awamu katika awamu ya pili.
Akizungumza kwa niaba ya Halmashauri ya Jiji Mstahiki Meya Sima Constantine Sima ameahidi kukamilisha ujenzi huu wa awamu ya pili kwa wakati na kuzingatia matumizi sahihi ya fedha hizo.
Akihitimisha sherehe hizi za makabidhiano,Katibu tawala wa Mkoa wa Mwanza amezitaka shule zote za Mkoa wa Mwanza zilizopata fedha hizi kutumia fedha zilizobaki kutumika kujenga au kutekeleza miradi inayoonekana na sio kufanya ukarabati ili kuondoa hoja za ukaguzi.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.