Balozi wa Finland Nchini Tanzania, Mhe.Theresa Zitting afanya ziara katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza yenye lengo la kuimarisha uhusiano kati ya Jiji la Mwanza na Jiji la Tampere pamoja na Taasisi za Nchini Finland.
Katika ziara hiyo, Mhe.Balozi Zitting amepokea taarifa ya maendeleo ya uhusiano kati ya Jiji la Mwanza na Tampere kisha kuahidi kuwa ofisi yake itatoa ushirikiano kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania katika kuwezesha shughuli zitokanazo na uhusiano kati ya majiji hayo.
Aidha, Mstahiki Meya wa Jiji Mhe.Sima C. Sima ameeleza umuhimu wa kushirikiana katika miradi ya maendeleo na kubadilishana uzoefu katika nyanja za kijamii na kiuchumi.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Bw. Jeremiah Lubeleje ameishukuru Serikali ya Finland kwa kuendelea kutoa fursa mbalimbali kwa Nchi yetu na kugusia baadhi ya manufaa yaliyopatikana kupitia uhusiano wa Majiji haya.
Naye Mratibu wa uhusiano wa Miji Dada (Sister cities) Halmashauri ya Jiji la Mwanza Bw. Billy Albert Brown amesema kuwa Halmashauri ya Jiji la Mwanza itaendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Miji rafiki iliyoko Nje ya Nchi katika kuchangia maendeleo ya jamii ya Mwanza kwenye sekta mbalimbali.
Vilelvile aliongeza kuwa Halmashauri ya Jiji itaendelea kushirikiana na ubalozi wa Finland katika kuendeleza uhusiano wak na Jiji la Tampere.
Ikumbukwe uhusiano wa Jiji la Mwanza na Tampere ulianza mwaka 1988 ambapo hadi sasa ni Zaidi ya miaka 37, na kufanikiwa kutekeleza shughuli mbalimbali ikiwemo kuliwezesha Jiji la Mwanza kufanya mapitio ya hiyari ya utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kuelekea safari ya 2050.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.