• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza City Council
Mwanza City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Orodha ya Viongozi Waliopita
      • Wenyeviti wa Halmashauri
      • Wakurugenzi
      • Wakuu wa Wilaya
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii
      • Uchumi, Mipango na Ufuatiliaji
      • Mazingira na Usafi
      • Fedha na Biashara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA,Habari na Uhusiano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria na Usalama
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Usafi wa mazingira na uhifadhi wa taka ngumu
    • Leseni
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Maji
  • Baraza la Madiwani
    • Orodha ya madiwani
    • Kamati za kudumu za halmashauri
    • Ratiba ya vikao
    • Mihtasari ya vikao vya baraza
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • TASAF
    • Mfuko wa Jimbo
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Waraka
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio Yajayo
    • Magazine

ELIMU YA FEDHA YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA JIJI LA MWANZA

Posted on: March 20th, 2025

Watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza wameshauriwa kujifunza kuhusu uwekezaji ili kuhakikisha kuwa baada ya kustaafu wanaendelea kuishi maisha mazuri kama walivyokuwa kazini.

Ushauri huo umetolewa na Afisa Masoko Mwandamizi, Kampuni ya Uwekezaji ya UTT – AMIS, Bw. Rahim Mwanga, March 20,25 katika ukumbi mkubwa wa Jiji wakati wa mafunzo ya elimu ya fedha yaliyotolewa kwa watumishi wa Halmashauri na Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha na Taasisi zake.

Aliongeza kuwa kustaafu hakupaswi kuwa chanzo cha matatizo ya kifedha, kwa mfanyakazi yoyote aliyekuwa analipwa mshahara bali iwe fursa ya kufurahia matunda ya kazi ya muda mrefu.

“Tukijijengea utamaduni wa kuwekeza mapema kutatusaidia sisi wafanyakazi kuepuka changamoto za kifedha baada ya kustaafu na kuwa na maisha ya uhakika”, alisema Bw. Mwanga.

Aidha aliwasisitiza wafanyakazi wote nchini kuhakikisha michango yao inalipwa kwa wakati na waajiri wao lakini pia watumie Mifuko ya Hifadhi ya Jamii inayotoa faida kubwa.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Bw. Erick Mvati, aliipongeza Wizara ya Fedha kwa kufika katika Mkoa wa Mwanza kutoa elimu ya fedha ambayo ni muhimu kwa wananchi ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Aliongeza kuwa elimu hiyo ikifika kwa wananchi wote katika makundi mbalimbali itasaida kupunguza matatizo katika jamii kwa kuwa wananchi wataelewa haki zao lakini pia watajua sheria mbalimbali zitakazowaongoza na kujiepusha na migogoro ya mikopo.

Naye Afisa Usimamizi wa Fedha, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Santley Kibakaya, alisema kuwa Wizara inaendelea na zoezi la utoaji elimu ya fedha kwa wananchi ili wafahamu fursa mbalimbali zinazopatikana katika Sekta ya Fedha.

Aliongeza kuwa Sekta ya Fedha imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali, kupitia elimu hiyo inayoendelea kutolewa, wataalamu hao wanapata fursa ya kusikiliza changamoto, ushauri na maoni yanayotolewa na wananchi kwa ajili ya kufanyiwa utatuzi zile ambazo zinatakiwa kufanyiwa utatuzi, ushauri na maoni kwa ajili ya kuboresha zoezi hilo kwa mikoa ambayo haijafikiwa.

Matangazo ya Kawaida

  • TANGAZO LA RATIBA YA KUINGIA KWA WAPANGAJI WA MAENEO MBALIMBALI YA SOKO KUU. June 29, 2025
  • TANGAZO LA MAPENDEKEZO YA SHERIA NDOGO ZA HALMASHAURI YA JIJI LA MWANZA July 10, 2024
  • MATOKEO YA USAILI WA KUANDIKA (MCHUJO) KADA YA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II - MWANZA JIJI April 29, 2023
  • KUITWA KAZINI NAFASI YA MEO III, MWANDISHI MWENDESHA OFISI II, RMA II na DEREVA II January 08, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA JIJI LA MWANZA KWA KUSHIRIKIANA NA RAILWAY CHILDREN AFRICA YAPANGA MIKAKATI YA KUKABILIANA NA WATOTO WA MTAANI

    June 26, 2025
  • HANANG' WAJIFUNZA MBINU ZA KUONGEZA MAPATO KUTOKA HALMASHAURI YA JIJI LA MWANZA KUPITIA STENDI KUU YA MABASI NYEGEZI

    June 10, 2025
  • DC AWATAKA WANANCHI KUSHIRIKI KATIKA UZINDUZI WA MIRADI

    June 02, 2025
  • MHE. MAKILAGI AONGOZA ZOEZI LA USAFI BUHONGWA KATIKA UZINDUZI WA WIKI YA MAZINGIRA

    May 31, 2025
  • Tazama Zote

Video

Ziara
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Mbalimbali
  • Kuhusu Sisi

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza
  • Vibali Kusafiri nje ya Nchi
  • ESS(Watumishi Portal)
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya wageni

freevisitorcounters's Website

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Barabara ya Balewa

    Sanduku la Posta: 1333,Mwanza

    Simu: +255 28 250 1375

    Simu ya Kiganjani: 0755741738

    Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.