Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mhe, Amima Makilagi amewataka wananchi wa Kata ya Luchelele kujitokeza kwa wingi kushiriki kampeni za uchaguzi wa viongozi wa Serikali za Mitaa zinazotarajia kuanza Novemba 20,2024.
Mhe, Amina Makilagi ameyasema hayo jana Novemba 19,2024 katika viwanja vya Nganza kata ya Luchelele alipofanya ziara yake ya kuhamasisha wananchi kujitokeza kuunga mkono Vyama vyote vya Kisiasa vitakavyokuwa vinanadi sera zake kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27,2024.
Aidha, Mhe Makilagi ameendelea kuueleza Umma wa wananchi kuwa kila mtu anahaki ya kuchagua na kuchaguliwa bila ubaguzi wa rangi, Kabila, Chama wala dini hivyo basi wanapaswa kuunga mkono vyama vyote kumi na tisa (19)vitakavyoshiriki kampeni za uchaguzi wakati wa kunadi sera.
Vilevile Mhe, Makilagi amevitaka yama vya siasa kuendesha kampeni kwa kuzingatia sheria na kanuni za uchaguzi na ametoa angalizo kwa atakaeenda kinyume na taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa sheria na Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, sheria itachua mkondo wake.
Naye Bw. Pascal Juma mkazi wa Luchelele ameunga mkono Juhudi zinazofanywa na Mkuu wa wilaya ya Nyamagana kwa kusimamia miradi inayotekezwa na Serikali ya awamu ya sita ya Dr Samia Suluhu Hassani, nakuwaomba Wananchi wenzake waungane kusikiliza sera zitakazokuwa zinatolewa na wafanya kampeni kwani itasaidia kupata kiongozi atakaleta maendeleo katika Mitaa na kata.
Mkuu wa wilaya ya Nyamagana, Mhe Makilagi amehitimisha kwa Kuwataka Wananchi kushiriki kampeni zenye amani kwani Nchi yetu ni ya amani na kuongeza kuwa hatamvumilia mtu yeyote atakayeonyesha viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.