Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mhe. Amina Makilagi amefanya mikutano ya hadhara katika Kata ya Igoma na Kata ya Mhandu kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero za wananchi.
Mikutano hiyo imefanyika keo Novemba 20, 2025 ambapo Wananchi walipata nafasi ya kueleza changamoto mbalimbali zinazowakabili, zikiwemo ukosefu wa ajira kwa vijana, gharama kubwa za uunganishaji wa miundombinu ya umeme ukilinganisha na vijijini, pamoja na tatizo la uchafuzi wa mazingira.
Aidha katika mikutano hiyo, DC aliwahakikishia wananchi kuwa serikali inaendelea kuchukua hatua kuhakikisha kero hizo zinapatiwa ufumbuzi wa kudumu. Aidha, alizisisitiza mamlaka husika kuendelea kuimarisha huduma ili kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo wanayostahili.
Akizungumzia suala la usalama na amani, DC aliwakumbusha wananchi umuhimu wa kudumisha utulivu katika maeneo yao. Aliwataka vijana kuepuka kujihusisha na vitendo vya uhalifu vinavyoweza kuhatarisha amani, akibainisha kuwa uhalifu ni kosa kisheria na kwamba mtu yeyote atakayebainika kukiuka sheria atachukuliwa hatua kali bila kuonea upande.
DC alihitimisha mikutano hiyo kwa kuwataka wananchi kuendelea kushirikiana na serikali katika kulinda miundombinu, kutunza mazingira na kutoa taarifa pindi panapotokea viashiria vya uvunjifu wa amani.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.