Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mheshimiwa,Mary Tesha Onesmo ametekeza zana za Uvuvi haramu katika ziwa Victoria. Zoezi hili limefanyika mapema jana katika Dampo la Buhongwa.
Akitoa Msimamo wa serikali wakati wa uteketezaji wa zana za Uvuvi Haramu Mheshimiwa Tesha amesema, Watu wote wanaojihusisha na Uvuvi haramu wataendelea kukamatwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria ili kuweza kulinda ziwa letu.
Aidha Mheshimiwa Tesha amewahasa wadau wa uvuvi kuendelea kuunga mkono serikali ya awamu ya Tano kutunza mazao ya Uvuvi kwa ajili ya vizazi vijavyo.
Akitoa taarifa juu ya operesheni hiyo, Mkuu wa Operesheni Kanda ya Mwanza Ndg. Gabriel. M. Mageni amesema Operesheni hii imezingatia sheria ya Uvuvi Na.22 ya Mwaka 2003 na sheria ya Mazingira ya Na.4 ya mwaka 2004.
“Tumefanya Ukaguzi kwenye viwanda Vitano vya kuchakata Samaki,Maeneo Saba ya kuchakata mabondo ya samaki na viwanda viwili vya kutengeneza nyavu na pia bandari za kupokelea mizigo kutoka Nje ya Jiji la Mwanza” amesema ndg Mageni
Aidha Ndugu Mageni amesema, zana zilizokamatwa ni pamoja na Nyavu za makila,(Gillnets) 5970,Makokoro ya dagaa 108, Nyavu za timba 106,makokoro ya Sangara 48, Samaki waliokamatwa kilogramu 1554, Mabondo ya sangara 39,Injini za boti 9,Kamba za kokoro mita 10,000, Kimea (Cast nets) 4,Watuhumiwa 4. Zana zote hizo zina gharama ya Tsh 293,400,000
Akitoa taarifa ya mapato yaliyokusanywa kutokana na mauzo ya mazao ya uvuvi na faini ndg Mageni amesema jumla ya Tsh 172,702,400 na tayari imelipwa Tsh 166,702,400 katika akaunti ya serikali.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.