Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mhe Amina Makilagi atoa wito kwa Wananchi kujitokeza kupata Chanjo ya saratani ya shingo ya Uzazi ambayo inatarajiwa kutolewa kuanzia tarehe 23 Aprili 2024 kwa wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza. Mhe Amina Makilagi amesema watakaochanjwa ni wasichana wenye umri kuanzia miaka 9 Hadi miaka 14 kwa Shule zote za Msingi na Shule za Sekondari.
Aidha Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana amesema wanatarajia kutoka Chanjo kwa wasichana 46,000 kwa wilaya ya Nyamagana hivyo ameomba Viongozi wote wa Dini, wenyeviti wa mitaa pamoja na Madiwani kutoa Hamasa kwenye jamii ili Wasichana wote wenye umri huo waweze kujitokeza kwa wingi kushiriki chanjo hiyo.
Mhe Makilagi amesema kwa Kanda ya Ziwa ugonjwa wa saratani ikiwemo saratani ya shingo ya Uzazi imesababisha vifo vingi vya wananchi wakina Mama wakiwa wahanga wakubwa wa tatizo hilo la Saratani.
Akizungumza Mganga Mkuu wa Jiji Dkt.Sebastian Pima amesema Chanjo ya H PV ilianza kutolewa nchini Mwaka 2014 na mwaka 2018 kama majaribio na ilitolewa kwa Nchi nzima, Dkt.Pima amesema Saratani ya shingo ya Uzazi hutokana na mabadiliko ya mfumo wa chembechembe au seli zilizoko katika shingo ya uzazi ya Mwanamke.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.