Chanjo ya Polio kuanza kutolewa Desemba 01.
Halmashauri ya jiji la Mwanza kupitia kamati ya afya ,leo tarehe 30 Novemba wamekutana na kufanya kikao cha pamoja juu ya chanjo ya matone ya polio kwa watoto kuanzia umri 0 mpaka wiki 59.
Kampeini hiyo inatarajia kuanza kesho tarehe 1 mpaka tarehe 4 Dec ikiwa ni awamu ya nne ya utoaji wa chanjo hiyo.
Akizungumza wakati akimuwakilisha mkuu wa wilaya ya Nyamagana ambaye ni mwenyekiti wa kamati hiyo Ndugu Yonas Alfred, amewaomba wajumbe wajitahidi kutoa elimu zaidi kwa jamii ili zoezi hili liweze kufanikiwa kwa asilimia kubwa.
Nae Kaimu Mganga mkuu wa hospital ya wilaya ya Nyamagana Dkt Gibson Simbulye, amewashukru wanakamati kwa kufanikisha zoezi la chanjo kwa awamu ya tatu, na amewaomba kutoa ushirikiano kwa awamu hii ya nne ili kufikia watoto wengi zaidi na kuwasisitizia wajumbe wafanyie kazi ushauri uliotolewa katika kikao hicho juu ya ufanikishaji wa zoezi hilo la kitaifa.
Ameongeza kua chanjo hiyo ni mhimu kwa watoto wadogo maana madhara yake ni makubwa kwa sababu kinga zao za mwili hazijaimalika, na mtoto asiyepata chanjo hiyo ni rahisi sana kuambukizwa na kuambukiza wengine.Na pia amesisitiza chanjo hiyo ni salama kabisa.
Nae Mratibu wa kamati ya kampein ya chanjo Nyamagana Ndg Makubi Gondela Ameeleza awamu hii wanalengo la kufikia watoto 119,815 ( laki moja na elfu kumi na tisa mia nane kumi na tano) wenye chini ya miaka mitano na kampeini hii itakua ni ya nyumba kwa nyumba na watafika maeneo mbalimbali yakiwemo mashule,vituo vya mabasi, nyumba za ibada. Pia ameomba wawahimize watu wajitokeze ili watoto waweze kupewa chanjo hiyo ya matone.
Pia wajumbe wa kamati hiyo wamesema watatoa ushirikiano wa kutosha na kuwafikia watoto wengi zaidi.
Kamati hiyo inajumuisha viongozi wa dini, viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama, madiwani ,wataalamu mbalimbali, pamoja na makundi mbalimbali ndani ya jamii.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.