Halmashauri ya Jiji la Mwanza na mkandarasi (Nyanza Road works) wasainiana Mkataba wa ujenzi wa Barabara za lami zenye urefu wa kilomita 4.4 na Ujenzi wa Dampo la Kisasa Buhongwa. Mkataba huo umesainiwa leo Katika Ukumbi Mkubwa wa Jiji la mwanza ambapo Ujenzi wote utagharimu Tsh Bilioni 15.9
Gharama hizo zinajumuisha ujenzi wa Barabara ya Mtakuja, Machemba , Sukuma na Umoja Pamoja na Ujenzi wa Dampo la Kisasa la Buhongwa
Akizungumza wakati wa hafla hiyo Fupi Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mheshimiwa Marry Tesha Onesmo amempongeza Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Ndg Kiomoni Kibamba kwa jitihada kubwa alizozifanya kukwamua mradi wa Dampo la kisasa ambao ulikuwa na hali mbaya hapo nyuma kiasi cha kuwafanya wafadhili kutaka kusitisha kutoa fedha “Nimshukuru sana Mkurugenzi ndiye aliyekwamua mradi wa dampo la Buhongwa na kufanya World Bank kutoa fedha kwa ajili ya Ujenzi wa Dampo” Amesema Mheshimiwa Tesha.
Aidha Mkuu wa wilaya ya Nyamagana amemtaka Mkandarasi aliyepata Zabuni ya Ujenzi wa Barabara za Lami na Ujenzi wa Dampo kukamilisha kazi kwa ufanisi mkubwa na kwa wakati “ninajua haikuwa kazi rahisi kupata hii zabuni ninaimani kubwa na kampuni yenu na ili hii imani kuwa ya maana ni vyema mfanye kazi hii kwa ufanisi mkubwa na mkamilishe kwa wakati mliokubaliana kwenye mkataba’’ amesema Mheshimiwa Tesha.
Mstahiki meya wa Jiji la Mwanza amesema kuwa wanaimani kubwa sana na kampuni ya Nyanza hivyo wanaamini kazi watakayoifanya itakuwa nzuri na ya viwango “Ninaimani kubwa na Kampuni ya Nyanza kutokana na kazi zenu nzuri mnazozifanya maeneo mengi nchini ni imani yangu kuwa kazi mtakayoifanya itakuwa nzuri na itaonesha thamani halisi ya fedha.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo Mbunge wa jimbo la Nyamagana Mheshimiwa Stanslaus Mabula, amesema kusainiwa kwa huo mkataba unaenda kulifanya Jiji la Mwanza kuwa Jiji safi na miongoni mwa majiji yenye madampo ya kisasa.
Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mheshimiwa Marry Tesha Onesmo akikata utepe kwenye Mkataba wa ujenzi wa Barabara za Lami Mji na Dampo la kisasa Buhongwa tayari kwa ajili ya kusainiwa
Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Ndugu Kiomoni Kibamba akisaini Mkataba
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mheshimiwa Stanslaus Mabula akitoa neno kwenye hafla fupi ya utiaji saini mkataba.
Mstahiki meya wa Jiji la Mwanza Mheshimiwa James Bwire akitoa hotuba fupi kwenye hafla fupi ya utiaji saini mkataba
Viongozi pamoja na wakuu wa Idara waliohudhuria kwenye hafla fupi ya kusaini Mkataba
Waheshimiwa madiwani ambao miradi inaenda kutekelezwa kwenye kata zao wakifuatilia kwa umakini kinachoendelea kwenye hafla hiyo
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.