Saturday 21st, December 2024
@TAMISEMI
KWA KUWA, Kanuni ya 21 ya Tangazo la Serikali Na. 572 ya tarehe 12 Julai, 2024 na Kanuni ya 22 ya Tangazo la Serikali Na. 571, 573 na 574 ya tarehe 12 Julai, 2024 zinatoa ukomo wa kuwa Madarakani kwa Mwenyekiti wa Mtaa na Wajumbe wa Kamati ya Mtaa katika Mamlaka za Miji siku saba kabla ya siku ya kuchukua fomu za kugombea uongozi ili kuweka mazingira yatakayowezesha uchaguzi wa nafasi hizo kuwa wa kidemokrasia, huru na wa haki;
HIVYO BASI, Kwa kuzingatia matakwa ya Sheria ya Serikali za Mitaa Sura 287 na Sura 288 na kanuni za uchaguzi wa serikali za Mitaa za mwaka 2024, na kwa kuzingatia marekebisho yaliyofanyika katika ratiba ya matukio ya uchaguzi wa serikali za mitaa na kutangazwa tarehe 15 Oktoba, 2024 ambayo yameanisha kuwa fomu za kugombea nafasi za uongozi zitaanza kutolewa kuanzia tarehe 26 Oktoba, 2024 hadi tarehe 1 Novemba 2024; Madaraka ya wenyeviti wa mitaa na wajumbe wa kamati za mitaa katika Mamlaka za Miji yatakoma kuanzia tarehe 19/10/2024. Nafasi za viongozi hawa zitajazwa kufuatia uchaguzi utakaofanyika tarehe 27/11/2024.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.