Mh Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Bi Mary Tesha Onesmo amevitaka Vikosi kazi vilivyoundwa kupambana na madawa ya kulevya katika wilaya ya Nyamagana kuwa na weledi mkubwa wakati wa kuendesha oparesheni ya kupambana na madawa ya kulevya.Hayo ameyasema leo kwenye kikao cha tathimini kilichofanyika katika Ukumbi wa “Gandh Hall” uliopo wilayani Nyamagana. Kampeni hiyo ilizinduliwa tarehe 21/03/2017
Aidha Bi. Tesha, amesema Oparesheni ya kupambana na Madawa ya kulevya isiwe sehemu ya kisingizio kwa watumishi wa Umma kutoendelea na majukumu yao ya kila siku “ Watu wamekuwa wakiniuliza Mheshimiwa zoezi hili litaisha lini ili tuweze kurejea kwenye shughuli zetu za kawaida” Bi Mary Tesha amesema.
Wakati huo pia Mheshimiwa amelitaka Jeshi la Polisi wilayani humo Kuwahudumia vizuri wananchi wanapofika vituo vya polisi kutoa taarifa mbalimbali za Uhalifu. “ Kuna baadhi ya Polisi wamezidi ukali wakimwona tu mwananchi amefika kituoni wanamwongelea kwa ukali na kuwaogopesha wananchi kueleza kero zao” Hivyo ni vyema kuwasikiliza na kuwaelekeza wananchi wanapofika Vituo vya polisi.
Mheshimiwa amewashukuru wadau mbali mbali waliohudhuria katika kikao hicho cha tathimini, akiviomba vyombo vya habari kutoa ushirikiano katika kampeni hii kwa kutoa muda wa hewani usiozidi saa moja kwa ajili ya elimu kwa umma na matangazo dhidi ya madawa ya kulevya.Katika oparesheni hiyo zaidi ya kesi 14 za madawa ya kulevya ziko mahakamani.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.