Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mhe, Amina Nassor Makilagi amefanya ziara ya kikazi na Kamati ya Siasa ya Wilaya pamoja na wataalam kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza Aprili 18, 2024 Wilayani humo, ambapo ziiara hiyo imehusisha kukagua miradi na kufanya tathimini ya miradi hiyo ambayo ikikamilika itachochea kwa kiasi kikubwa kukua kwa Sekta ya Uchumi katika Wilaya ya Nyamagana na Nchi kwa ujumla, sambamba na kuongezeka kwa kiwango kikubwa cha pato la Taifa.
Katika Ziara hiyo Mhandisi Abraham Msina, Msimamizi wa ujenzi wa Gati bandari ya kaskazini kata ya Nyamagana ameieleza Kamati pamoja na wataalam kuwa uboreshaji na upanuzi wa mradi wa bandari utagharimu shilingi billioni 18.6. Mradi huo ulianza terehe 3/05/2024 na unatarajiwa kukamilika tarehe 2/11/2024 na utekelezaji wake umefikia 27% ikiwa ni pamoja na ujenzi wa maegesho ya meli na miundombinu mingine bila kusahau ujenzi wa jengo la abiria na mizigo kutokana na kwamba meli itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 1200 na mizigo zaidi ya Tani 400 hivyo uchumi utapanda kwa kiasi kikubwa baada ya mradi kukamilika.
Sambamba na Mradi wa Bandari, Kamati na Wataalamu hao wameutembelea mradi wa Maji uliopo katika Kata ya Butimba ambao umetekelezwa kwa asilimia 100 kwa ushirikiano kati ya Wadau na shirika la Maendeleo la Ufaransa, Pamoja na Benki ya Uwekezaji ya Ulaya.
Akizungumzia mradi huo Meneja wa mradi Mhandisi Celestine Mahubi amesema, “Mradi huu wa ujenzi wa uondoaji taka katika Gereza la Butimba umetekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na Wadau wa maendeleo kutoka Shirika la Maendeleo la Ufaransa pamoja na Bank ya uwekezaji ya Ulaya na umegharimu shilingi billioni 1,969,863 ,543. Ambao ulianza Mei16,2023 na unatarajiwa kukamilika Juni 8,2024. Hivyo uwekezaji huo umesaidia kuboresha maji katika Jiji la Mwanza, na kuhakikisha Usalama wa matumizi ya maji ya Ziwa Victoria, kwa kuhakikisha uondoshaji wa maji taka upo katika Mazingira ya kuhifadhiwa na kusaidia wanufaika 4000 ikiwa ni pamoja na wafungwa na wafanyakazi wa Gereza la Butimba.”
Naye, Mhandisi Robert P. Lupoja Mkurugenzi usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira MWAUWASA katika taarifa yake fupi ya mradi wa maji Kata ya Luchelele, ameieleza kamati ya siasa kuwa upanuzi wa mambomba ya maji utanufaisha mitaa yote mitatu ya Luchelele nakuihakikishia kamati ya siasa na wataalam kuwa mradi utaisha kwa wakati.
Aidha, kwa upande wa Mradi wa barabara ya Tactic yenye kilometa takriban 14 kutoka Buhongwa hadi Igoma inayojengwa Buhongwa chini ya usimamizi wa TARURA, na Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa gharama ya shilingi Bilioni 22 unatalajiwa kukamilika kwa wakatiFeb,2025 sambamba na ujenzi wa Shule 4 ambazo ziko karibu na Mradi. Amesema Jane Madulla Mhandisi Mkuu wa TARURA-Mwanza.
Aidha, Mwenyekiti wa CCM Wilaya Mhe, Peter Bega, amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana kwa kuendelea kusimamia Miradi kwa weredi mkubwa na kumsihi kutowafumbia macho wanaomuangusha na kumtaka kuwachukulia hatua kwani kufanya hivyo kutaharakisha baadhi ya miradi ambayo bado inatekelezwa kukamilika kwa wakati na ametoa pongezi kwa Muheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dr, Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutuwezesha kwa kumwaga Fedha kwenye miradi ya kimkakati na kuahidi kutomuangusha bali wao kama Chama watahakikisha hawamuangushi ili miradi yote itekelezwe kwa wakati na kuisha kwa wakati.
Mkuu wa wilaya ya Nyamagana alihitimisha kwa kuiahidi Kamati ya siasa kuwa yote waliyoadhimia katika ziara atayafanyia kazi ili miradi imalizike kwa wakati.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.