Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mhe.Amina Nassor Makilagi katika kikao chake na waandishi wa habari kilichofanyika leo tarehe 8/03/2024 kwenye ofisi yake ameweka bayana bei elekezi ya sukari kwa wananchi na wafanyabiashara wa wilaya ya nyamagana.
Mhe. Amina Nassoro Makilagi amewataka wafanyabiashara wa sukari kufuata yale yaliyoadhimiwa kwenye kikao alichokaa na wafanyabiashara hao. Ikiwa ni pamoja na kufuata sheria iliyowekwa na kutoa risiti ya manunuzi ya sukari kwa bei elekezi kwa mujibu wa sheria na 251, iliyotolewa katika tangazo na 40A la tarehe 23/01/2024.
Nakuongeza kuwa wafanyabiashara hao wa jumla na rejareja wahakikishe wanauza kulingana na bei elekezi iliyotolewa na bodi ya sukari ambayo kwa bei ya jumla ni 2650 hadi 2800 na rejareja ni 2800 hadi 3000. Lakini pia wafanyabiashara hao watakiwa kubandika tangazo la bei katika maeneo ya biashara zao ili wananchi wajue bei halisi ya sukari.
Pia, Mkuu wa wilaya ya Nyamagana amemuagiza Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza kuhakikisha anawasimamia watendaji wa kata, serikali za mitaa na maafisa kilimo wanaosimamia bidhaa kuhakikisha wanasimamia kikamilifu utekelezaji wa agizo Hilo ili kupunguza ukali wa mfumuko wa bei wa bidhaa zingine, kwani itasaidia kupunguza ukali wa maisha kwa mwananchi.
Aliongeza kuwa kwa watakaokiuka na kushindwa kusimamia agizo Hilo washughulikiwe kupitia sheria namba 251 kifungu kidogo cha 6 ili kila mtu atimize wajibu wake.
Mkuu wa wilaya ya Nyamagana amewaeleza waandishi wa habari kuwa kazi ya serikali ni kuwatumikia, kuwasikiliza, na kutatua changamoto za wananchi ikiwemo hii ya sukari, hivyo kuamua kutoa elimu kwa wananchi kuhusu bei elekezi ya bidha hiyo ili wasiibiwe au kushurutishwa na wafanyabiashara ikiwemo kuwalazimisha wauzaji wa rejareja kununua bidhaa nyingine ili apate sukari.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.