Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Ndg John Mongela amewataka wafanyabiashara wanaofanya biashara kandokando ya Barabara eneo la Buhongwa kutoka na kupisha mkandarasi kutengeneza stendi ya magari madogo maarufu Kama Daladala.Mkuu wa Mkoa ameyasema haya alipotembelea eneo la stendi ya magari madogo Buhongwa
Aidha Mkuu wa Mkoa amesema maeneo yale si salama sana kwa wafanyabiashara hao kwani ni sehemu ambapo magari makubwa upita na hivyo lolote likitokea watu wanaweza adhiririka maeneo hayo.
Hata hivyo Ndg Mongela amepiga marufuku wafanyabiashara hao kuanza kuvamia maeneo ya Shule na kuweka vibanda vya biashara
Alipokuwa anaongea na Wananchi wa Maeneo hayo Mheshimiwa Diwani wa Kata ya Buhongwa Ndg kabadi aliwaambia wananchi wa maeneo hayo kuwa ni vyema wapishe maeneo hayo kwani ni hatari kwa ajili ya usalama wao. Aidha ndg kabadi alisema wao kama kata watawapanga wafanyabiashara wa maeneo hayo kwenye eneo la Mlima wa Nyuki. Mheshimiwa Kabadi aliendelea kumwomba mheshimiwa Mkuu wa mkoa kuwapa siku mbili wafanyabiashara wa maeneo hayo ili waweze kuondoa meza zao ombi ambalo lilikubaliwa na Mheshimiwa Mkuu wa mkoa wa mwanza ndg Mongela
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.