Kamati ya Fedha na Uongozi yatembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri ya Jiji la Mwanza ikishirikiana na Wananchi.
Kamati hiyo ya Fedha ambayo iliongozwa na Mstahiki meya wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza Ndg James Bwire. Walikagua mradi wa Ujenzi wa Tenki kubwa la maji uliopo Fumagila uliotumia zaidi ya Milioni 800, Mradi wa ujenzi wa Nyumba mbili za kuoshea magari ya Taka na Mizani eneo la Dampo wenye thamani zaidi ya milioni 400, Ujenzi wa zahanati eneo la Bulale wenye thamani zaidi ya milioni 30, Ujenzi wa Vyumba vitatu (3) vya madarasa eneo la Nyasubi kata ya Mkolani wenye thamani zaidi ya milioni ishirini (20), Ujenzi wa Ofisi ya Walimu shule ya Msingi Sweya Kata ya Luchelele wenye thamani zaidi ya Milioni ishirini (20), Ujenzi wa Vyumba viwili (2) vya madarasa Shule ya Msingi Mkuyuni kata ya Mkuyuni wenye thamani zaidi ya milioni ishirini (20) Ujenzi wa Ofisi ya Mtaa Bugarika Kaskazini kata ya Pamba wenye thamani zaidi ya milioni kumi (10), Ujenzi wa ofisi ya serikali ya Mtaa wa Maendeleo kata ya Isamilo wenye thamani zaidi ya milioni 10.
Aidha miradi mingi ipo katika hali ya kukamilika isipokuwa ujenzi wa zahanati ya Bulale na Ujenzi wa Madarasa Matatu Shule ya Msingi Nyasubi ambapo mpaka sasa Maboma ndio yamekamilika.
Mhe Meya alipokuwa katika eneo la Dampo alisema ni vyema miradi inayotekelezwa kusadifu thamani ya hela ya miradi husika “Value for money”
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.