Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Mwanza limefanya ziara ya mafunzo katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya yenye lengo la kubadilishana uzoefu wa utendaji kazi katika maeneo mbalimbali ambapo katika ziara hii iliyofanyika kuanzia tarehe 16 - 20 Desemba 2019 imetoa fursa kwa Halmashauri zote mbili kujifunza na kubadilishana uzoefu katika maeneo ya:-
Uendeshaji na usimamizi dampo la kisasa, Uanzishwaji na uendeshaji wa shule za English Medium zilizo chini ya Halmashauri, Usimamizi na uendeshaji wa soko ya kisasa, Ukusanyaji na uendeshaji wa vyanzo vya mapato, uendeshaji wa Shughuli mbalimbali za uchaguzi na uendeshaji na uzimamizi wa Redio ya Halmashauri.
Akitoa neno la ukaribisho Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya ameushukuru uongozi wa Halmashauri ya jiji la Mwanza kwa kuchagua kuitembelea Halmashauri ya jiji la Mbeya bila kujali umbali na kuahidi kuendeleza ushirikiano baina ya Halmashauri hizo mbili ambapo kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mbeya alishukuru Zaidi kuwezesha kukutana na baadhi ya watumishi na Waheshimiwa aliofanya nao kazi akiwa Halmshauri ya jiji la Mwanza na kuwakaribisha Mbeya.
Kwa upande wake Kaimu mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza na Kaimu Mkururugenzi wa Halmashauri ya Jiji la mwanza wametoa shukrani kwa yote ikiwemo mapokezi mazuri na kuwakaribisha wana Mbeya kama halmashauri kuja kuitembelea Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.