Mh Wiliam Lukuvi ameyasema hayo leo alipozuru Halmashauri ya Jiji la Mwanza na kukutana na watumishi wa Idara ya Mipangomiji kwa kuziagiza Halmashauri zote nchini kulifanya zoezi la ukusanyaji kodi ya ardhi kuwa la lazima na sio ziada ili kuongeza mapato ya serikali “serikali sasa inatoa elimu bure nchini kote kwa kuleta ruzuku mashuleni fedha hizo ndizo hizi mnazozikusanya” amesema Lukuvi
Katika kikao chake hicho na watumishi katika Ukumbi Mkubwa wa Halmashauri, Mheshimiwa waziri ameipongeza Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa kazi kubwa walioifanya kwa kupima zaidi ya viwanja 19000 na kupunguza kero za wananchi zinazohusiana na ardhi tofauti ilivyokuwa huko nyuma.
Aidha Mheshimiwa Lukuvi amezitaka Taasisi zote za serikali kwa mwaka huu kupima maeneo yao na kuyawekea alama zinazoeleweka ili kuzuia migogoro mbalimbali inayojitokeza kati ya wananchi na taasisi husika kwa watu kuvamia maeneo mbali mbali yaliyotengwa na Taasisi hizo.
Hali kadhalika Mheshimiwa Waziri amewataka Maafisa wote wa ardhi kuhakikisha wanapotoa hati za ardhi majina ya wamiliki yanafanana na majina yaliyosajiliwa kwenye vitambulisho vya Taifa kuepuka watu kukwepa kodi za serikali.
Mwisho Mheshimiwa waziri amesema wapo katika hatua ya mwisho ya kuandaa utaratibu wa kuwatambua watu wenye viwanja au mashamba ambayo yapo mjini na hayajapimwa kulipa kodi ya viwanja vyao.
Akihitimisha katika kikao hicho Mheshimiwa Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Bi Mary Tesha Onesmo amemuhahidi Mheshimiwa waziri kuhakikisha maagizo yote aliyoyatoa yanatekelezwa
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.