Waziri wa ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi mhe; William Lukuvi ameagiza watendaji na viongozi wote wa mitaa kuhakikisha wanasimamia taratibu na Sheria za ujenzi mijini ili kuepuka ujenzi holela na uvamizi wa ardhi.
Amesema mji wowote ulio na viongozi wanaozingatia sheria hauwezi kuwa na wananchi wanaolalamikia dhuruma ya ardhi zao,na pia mji wowote uliopangwa unazingatia taratibu za ujenzi kisheria kupitia mamlaka za Halmashauri kitengo Cha mipango miji.
"Ujenzi wowote unaofanyika mjini,unapaswa kuwa na vibali vya ujenzi,ambapo wataalam kutoka katika Halmashauri watafika eneo la ujenzi kulikagua na pia kushauri aina ya ujenzi kulingana na ramani na matumizi yaliyopangwa na serikali"alisrma Lukuvi.
Agizo hili limetolewa Leo alipokuwa anazindua awamu ya tatu ya mpango kabambe wa Jiji la Mwanza wenye maoteo ya kuliendeleza Jiji la Mwanza kwa kipindi Cha mwaka 2015 mpaka 2035.
Akizindua mpango huu kabambe waziri Lukuvi ameutaka uongozi wa serikali ya Mkoa wa Mwanza kwa usimamizi wa Mheshimiwa Mhandisi Robert Gabriel (Mkuu wa Mkoa wa Mwanza) kuhakikisha mpango huu unakilika kwa wakati kama ulivyo kwenye makaratasi.
Mpango kabambe wa Jiji la Mwanza ambao pia unazihusiaha Halmashauri za Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela una lengo la kuboresha miji hiyo kiuchumi,miundo mbinu na huduma bora za kijamii ikiwa ni huduma za kisasa kwa kuzingatia ramani na mpango uliowekwa na serikali kupitia Halmashauri zake.
Akitoa wasilisho la mpango huu kabambe Afisa Mipango Miji Ndg; Mosses Seleki amesema kulingana na maoteo ya ongezeko la idadi ya watu na mahitaji mengine ya kijamii Halmashauri zimelazimika kuandaa mpango huu kabambe kwa lengo la kujitosheleza kimahitaji ya ardhi na huduma muhimu za kijamii.
Akifunga mkutano huo, Mheshimiwa Lukuvi amesifu jitihada za Halmashauri ya Jiji la Mwanza zakujenga madarasa ya ghorofa huku akizitaka Halmashauri zote nchini kuiga utaratibu huo ili kuweka matumizi mazuri ya ardhi katika maeneo ya umma.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.