Kutokana na somo la Kiingereza kuwa changamoto katika Shule za Msingi Halmashauri ya Jiji la Mwanza imechukua hatua stahiki za kutoa mafunzo kwa walimu 40 kwa lengo la kuwataka baada ya mafunzo hayo nao kutoa elimu kwa walimu wenzao wanaofundisha somo la kingereza shule za msingi.
Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza Bw. Mussa Ally Lambwe ameyasema hayo mnamo Mei 5,2025 huku akiwataka Walimu wanaopewa mafunzo kuwa makini kwa sababu watasambazwa katika kanda nne ambazo ni igoma , Sahara , Iseni na Buhongwa na wao kutoa elimu kwa walimu wa masomo ya kiingereza Shule zote za Msingi zilizopo wilaya ya Nyangana.
Naye Afisa Elimu Msingi Mkoa wa Mwanza Bw.Martin Nkwabi ametoa shukrani kwa Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa kuona umuhimu wa kutoa mafunzo kwa Walimu wa somo la kiingereza ili kuwapatia maarifa ya kutosha na wao waweze kuwajengea uwezo walimu wenzao kwa kuwafundisha mbinu za kuwawezesha wanafunzi kuweza kufaulu somo hilo ambalo ni changamoto katika ufaulu kwa shule za Msingi.
“ Somo la kiingereza limekuwa ni changamoto katika ufaulishaji kwaio kuwafundisha walimu kuwa Mahiri katika ufundishaji kutapelekea ufaulu wa somo hili la kingereza kuongezeka hivyo nishukuru Halmashauri ya Jiji la Mwanza kuona umuhimu wa kuwapa uwezo walimu wa kuwafundisha walimu wenzao “
Vilevile, Mwl.Ramadhani Matibwa, Mwezeshaji wa mbinu za Kufundishia somo la kiingereza, ameeleza mbinu hizo ni pamoja na kutumia kingereza wakati wa kufundisha na hata kama mwanafunzi hajaelewa Mwalimu asitumie kiswahili atafute mbinu mbadala, kutumia kiingereza kwenye mazingira ,vitu vinavyoonekana na nyimbo ili kujenga uwezo na ufanisi kwa wanafunzi na kuwatathimini uelewa wao kabla hawajafanya mitihani ya somo la kungereza.
Aidha, Mwl. Fubusa Kibabala, ambaye ni mwenyekiti wa Walimu wakuu Shule za Msingi Mkoa wa Mwanza ameunga mkono mafunzo haya kwa walimu ili kuhamasisha Walimu wakuu wawaruhusu walimu wao kuja kupata mafunzo kwa kile kilichofundishwa na kuwasimamia kwa vitendo mashuleni ili kuleta tija kwa wanafunzi na kuinua viwango vya ufaulu katika somo la kiingereza.
Pia, Mwl.Thereza Boniphace kutoka shule ya Msingi Mahina. Akizungumza kwa niaba ya walimu wenzake waliopata fursa ya kupata mafunzo haya ameshukuru kwani yatawajengea uwezo na umahili wa kuwafundisha walimu wenzao mbinu mbalimbali za ufundishaji ili wazitumie kuwafundisha wanafunzi kwa lengo la kuongeza ufaulu wa somo la kiingereza kwa Shule za msingi.
Licha ya kupata mafunzo kutoka kwa wawezeshaji pia walimu hao walipata wasaa wa kubadilishana uzoefu wa shule za mchepuo wa kiingereza (English Medium) na zile za Mchepuo wa kiswahili ( Swahili medium) kitu kilicholeta umoja miongoni mwao katika ushirikiano wa zoezi zima lilivyoendeswa na wawezeshaji.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.