Mwenge wa Uhuru 2025 umefika katika Wilaya ya Nyamagana Jumatatu, Agosti 25, 2025, ukitokea wilayani Ukerewe. Mapokezi yake yamefanyika katika Uwanja wa Nyamagana.
Akipokea Mwenge huo, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mhe. Amina Makilagi amesema kuwa jumla ya miradi saba yenye thamani ya shilingi bilioni 50.2 itapitiwa. Miradi hiyo inahusisha sekta mbalimbali ikiwemo: Maji (Ujenzi wa tenki la Maji safi), Vizimba vya samaki, Ellimu (Vyumba 11 vya madarasa na matundu 28 ya vyoo), Barabara ya Zege, Afya ( kituo cha Afya Mkolani), Usalama wa wananchi (kituo cha polisi Nyegezi), na Maeneo ya umma.
Aidha, Mhe. Makilagi amewahimiza wananchi kujiandaa kushiriki Uchaguzi Mkuu Agosti 29, 2025 kwa amani na utulivu, akisisitiza kaulimbiu ya Mwenge wa Uhuru mwaka huu isemayo:
“Shiriki Uchaguzi Mkuu 2025 kwa Amani na Utulivu.”
Kwa upande wake, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025, Ismail Ally Ussi, amepongeza viongozi wa Wilaya ya Nyamagana wakiongozwa na Mhe. Makilagi, akisema anaamini miradi yote itakayopitiwa na Mwenge imekamilishwa kwa viwango bora na inaleta manufaa kwa wananchi.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.