Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Mamlaka za serikali za Mitaa Kanda ya Ziwa Victoria (LVRLAC) BILLY ALBERT BROWN Ameongoza kikao cha Nishati safi ya kupikia kwa wanawake viongozi kutoka kanda ya ziwa ikiwemo Wakurugenzi, Madiwani na Wataalamu mnamo Desemba 19,2024 katika ukumbi wa Gold Crest.
Ameendelea kuwasihi wanawake kutumia fursa waliyoipata yakuja kujifunza kwa wadau ili wawe mabalozi wazuri wa kuhamasisha matumizi ya nishati safi yakupikia katika maeneo yao wanayoongoza ili kupunguza hewa ukaa ikiwa ni pamoja na uchafuzi wa mazingira.
Mheshimiwa Diwani na Mwenyekiti wa mtandao wa wanawake Jumuiya ya Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania ( LVRLAC) Mariam Mafutaa, Amewaomba wadau waliyoalikwa kutoa elimu ya bidhaa za majiko wanazouza ikiwa ni mkakati wa kuhamasisha kutumia nishati safi kuwa na bei ambayo watanzania wataweza kumudu ili kupunguza uchafuzi wa mazingira.
Vilevile amewataka wanawake viongozi wakirudi kwenye Halmashauri zao kupaza sauti kwa wananchi kwa kutoa elimu kuhusu nishati safi yakupikia hususani wanawake ambao ndiyo wapishi wakubwa kwenye famili.
Naye Mathias Luhenga mdau kutoka kampuni ya Ecoa-Burn Manufacturing ametoa elimu kwa Wanawake viongozi kuhusiana na matumizi ya bidhaa zao za majiko katika harakati za utunzaji wa mazingira ambapo wameweka punguzo la 18% kutokana na kwamba jiko linauzwa 300,000/= baadala ya 430,000/= na lengo kuu ikiwa nikutaka kila mtanzania amiliki jiko lisilosababisha uchafuzi wa mazingira.
Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mamlaka za Serikali za Mitaa Kanda ya ziwa Victoria (LVRLAC)Mstahiki Meya wa Musoma william Gumbo amehitimisha kwa kuwataka wanawake viongozi kuwa msitari wa mbele kueneza elimu ya nishati safi ya kupikia ili kuondokana na hewa ukaa inayoleta athari kwenye Mazingira yetu yanayotuzunguka ikiwa ni pamoja na kuunga Mkono Juhudi zinazofanywa na Rais wa Tanzania kwa kutoa ruzuku kwenye majiko ili kila mtanzania aweze kutumia nishati safi.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.