.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mhe, Amina Makilagi amewahimiza wananchi wa Kata ya Mahina kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi la upigaji kura na kuwachagua viongozi watakaowaongoza.
Makilagi ametoa wito huo Jana Novemba 18,2024 wakati akiendelea na ziara ya kata kwa Kata na kuongeza kuwa ni haki ya Kila mtanzania mwenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea kushiriki zoezi la uchaguzi utakaofanyika Novemba 27, 2024.
Vile vile Mhe, Makilagi amewasisitiza wananchi kushiriki kampeni za wagombea wa vyama vyote 19 vya siasa zitakazoanza tarehe 20-26 Novemba 2024 ili kusikiliza sera za Kila mgombea na kuchagua kiongozi bora.
Aidha amekemea kampeni zisizo za staha kwa wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi wakati wa kunadi sera zao badala yake wafuate kanuni, taratibu na sheria ili kuhakikisha Uchaguzi unafanyika kwa amani na utulivu.
Katika hatua nyingine Makilagi alipata nafasi ya kuwaeleza wananchi juhudi mbalimbali za kuondoa changamoto kwa wananchi zinazofanywa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dr. Samia Suluhu Hassan ambapo amezitaja baadhi ya juhudi kuwa ni uboreshaji wa sekta ya Elimu, Afya, Miradi ya maji pamoja na muindombinu ya usafirishaji.
Naye Bw. Edward Ryoba Kisunte mkazi wa Mahina amempongeza Mhe, Mkuu wa wilaya kwa juhudi alizonazo za kiutendaji za kuhakikisha anasimamia Miradi yote ya maendeleo kupitia serikali ya awamu ya sita ampapo kwa Wilaya ya Nyamagana miradi mingi imetekelezwa na matunda yake yanaonekana.
Mwisho amewashukuru wananchi wote kwa kujitoa na kushiriki mkutano huo na kuwasisitiza wananchi wote waliojiandikisha Katika daftari la makazi washiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.