Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa (ALAT) kutoka Mkoa wa Mara Mhe. Daniel Komote amewaongoza wajumbe wa Jumuiya hiyo katika ziara ya kujifunza ndani ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza, mnamo Februari 11, 2025.
Katika ziara hiyo, wajumbe wamejifunza mbinu mbalimbali za ufanisi katika usimamizi wa miradi ya maendeleo na ukusanyaji wa mapato huku lengo kuu likiwa ni kubadilishana uzoefu na kujenga uwezo wa kuboresha utendaji katika Halmashauri zao.
Katika mafunzo hayo wajumbe wamepata nafasi ya kujifunza juu ya mfumo wa ukusanyaji mapato (Balozi System) ambao unatumiwa na Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa kutumia Mabalozi kuwatambua wafanyabiashara katika mitaa yao.
Aidha Mhe. Emmanuel Machumwa kwa niaba ya wajumbe ameipongeza Halmashauri ya Jiji la Mwanza na kuahidi kufanyia kazi mbinu hiyo kupitia vikao vyao vya kikanuni na kuona namna ya kuwatumia mabalozi katika kukusanya mapato.
Katika hatua nyingine wajumbe wamepata nafasi ya kutembelea miradi inayotekelezwa na Halmashauri ikiwemo mradi wa ufugaji wa samaki kwa njia ya Vizimba (Luchelele), mradi wa Ufyatuaji tofali pamoja na eneo la kutunzia taka ngumu( Dampo) Buhongwa.
Ziara kama hizi ni muhimu kwa viongozi wa serikali za mitaa ili kuimarisha utendaji wao na kuhakikisha huduma bora kwa wananchi.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.