Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Nyamagana ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya Siasa ya Wilaya ndugu Zebedayo Athumani, Leo tarehe 11/8/2022 ameongoza ziara hiyo akiambatana na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mhe. Amina Makilagi , Mbunge wa Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula, Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, wajumbe wa kamati ya Siasa ya Wilaya na Wataalamu mbalimbali wa wilaya ya Nyamagana.
Katika ziara hii miradi mbalimbali imekaguliwa ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa 14 na ofisi 3 katika shule ya Msingi Bulale, Ujenzi wa jengo la OPD zahanati ya Shadi kata ya Luchelele , mradi wa ujenzi wa Barabara SAUT - Luchelele na Shadi ya urefu wa kilometa 1.300 na mita 200 huko Luchelele Shadi na ujenzi wa jengo la OPD na Mashimo ya maji taka katika hospitali ya Wilaya ya Nyamagana.
Akizungumza na wajumbe wa kamati ya Siasa ya Wilaya , Wataalamu na Viongozi wa eneo la Bulale , Mhe. Mwenyekiti amempongeza Mkuu wa Wilaya Mhe. Amina Makilagi Kwa kuja na wazo zuri la kupambana na changamoto ya upungufu wa madarasa na kuweka mazingira rafiki ya ufundishaji na ujifunzaji shuleni Kwa maendeleo na ufaulu Bora.
Katika kufafanua wazo hilo, Mheshimiwa Amina Makilagi ameeleza kuwa baada ya wazo hilo lililoambatana na kauli mbiu "Uzalendo Kwanza, kazi iendelee Wilaya ya Nyamagana" aliwashirikisha Wadau mbalimbali wa Elimu na hivyo kupata mwitikio mkubwa na wadau mbalimbali wameshiriki Kwa Mali na nguvu pia.
Aidha, Mheshimiwa Stanslaus Mabula Mbunge wa Nyamagana amewashukuru na kuwapongeza Viongozi wote Kwa ushirikiano na kwamba Kwa kufanya hivyo tunaweza kufika mbali pia ameshauri uongozi wa Chama cha Mapinduzi kushiriki kuongeza hamasa zaidi katika zoezi hili.
Sanjali na hayo, Mhe. Mwenyekiti wa kamati ya Siasa ya Wilaya ya Nyamagana amewapongeza Wataalamu Kwa kufikia hatua nzuri katika ujenzi wa zahanati, Barabara na hospitari ya Wilaya ya Nyamagana. Kwamba ukamilifu huo utasaidia watu wengi kupata huduma na katika mazingira mazuri.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.