Halmashauri ya Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela wakishirikiana na Shirika la Maendeleo la Ubelgiji ENABEL na wawezeshaji wa mafunzo ya Digital skills " DIGIFY" ENNOVATE VENTURE wametoa mwongozo wa jinsi ya kujiunga na mafunzo hayo kwa njia ya mtandao ( online learning) kwa vijana 65 walioshiriki kupata taarifa ( info session) katika ukumbi wa mafunzo ofisi ya Mganga Mkuu Mwanza. Mafunzo hayo yataanza mwezi Septemba, 2024.
Akizungumza Ndg.Daniel Kasongi Meneja na Mtaalam wa ICT kutoka Ennovate Venture amesema program hiyo ya "Digify Skills lab" ni mahususi kwa ajili ya vijana kujiendeleza katika fani mbalimbali ambazo zitawawezesha kujiajiri wenyewe lakini pia kuwakutanisha na wazoefu wa fani hizo ilikuwajenga na kuwasaidia kupata ajira au namna ya kujiajiri wenyewe kama freelancer.
Aliongeza kuwa "ili kupata mafunzo hayo vijana wanatakiwa kujisajili mtandaoni kwa kutumia wavuti ya bit.ly/DigifyMwanza . Lakini pia mafunzo hayo yataendeshwa kidigitali hivyo vijana mnatakiwa kuwa na vifaa vya tehama kama Tanakilishi Mpakato (Laptop), Simu janja (Smartphone) au Kishikwambi (tablet)" .
Waratibu wa mradi wa Green and Smart Cities project, Ndg. Fanuel Kasenene ( Mwanza Jiji) na Ndg. Ahmed Sakibu ( Manispaa ya Ilemela) wamewasisitiza vijana waliohudhuria kuchangamkia fursa hiyo ya mafunzo yanayotolewa bila malipo yoyote kwa sababu Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya wameona kuna umuhimu mkubwa wa kuwajengea uwezo vijana kuendana na mabadiliko ya teknolojia na fursa za kidigitali.
Vijana kutoka Wilaya ya Nyamagana wakishiriki kikao taarifa (Info Session) kuhusu mafunzo ya Digify skills
Vijana kutoka Manispaa ya Ilemela wakishiriki kikao taarifa (Info Session) kuhusu mafunzo ya Digify skills
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.