Akizungumza na wananchi wa kata ya Mkolani Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mhe.Amina Makilagi m namo April 3 , 2025 katika ziara yake kata ya Mkolani ameeleza kuwa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan imejipanga ipasavyo kwenye masuala ya kiusalama katika Jiji letu la Mwanza hasa ndani ya wilaya yetu ya Nyamagana.
" niwatoe shaka wananchi wa kata hii ya mkolani ambayo ipo katika wilaya ya nyamagana suala la kiusalama ni safi asitokee mtu yoyote yule Kuja kutuchafulia amani yetu na usalama wetu tulionao "
Aidha , katika mkutano huo wa hadhara Mhe.Amina Makilagi ametolea ufafanuzi wa changamoto ya Barabara kutoka password - Nyegezi kuelekea Msikitini eneo la Tenkini.
" .Ni kweli Barabara hii imekuwa ni changamoto kutokana na kusaahulika kwenye bajeti ya Fedha za ndani hivyo niwatake Tarura kwenye bajeti ya Fedha ya Mwaka 2025 Mpango huu wa ujenzi wa Barabara hii ya password kuja Msikitini - Tenkini muiweke Ili kupitia mapato ya ndani iweze kukamilika"
Katika ziara hiyo Mkuu wa wilaya ya Nyamagana ameueleza umma kuhusu mafanikio tuliyoyapata katika uongozi huu wa awamu ya sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan imefikia wapi na inafanya nini Mhe. Amina Makilagi amesema,
" Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imetoa Shilingi Bilioni 5 Kukamilisha Ujenzi wa Daraja la Mkuyuni na Upanuzi Wa Barabara ambapo Mvua ikinyesha inakuwa ni changamoto kubwa hivyo Kwa kutambua umuhimu wa Barabara hiyo na Kuepukana na Foleni Serikali hii imetoa bilioni 5 Kwa ajili ya matengenezo ya Barabara hiyo na utanuzi wa Daraja "
Ziara hii ya Mkuu wa Wilaya imekuwa ni sehemu ya Kusikilizwa Kwa kero Mbalimbali za Wananchi na Kuzitatua Kwa kadri inavyowezekana bila kujali dini , jinsia Wala kabila .
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.