Mafunzo ya siku mbili kuhusu uandaaji wa mpango na bajeti kwa Maafisa Bajeti na Wakuu wa Idara katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza yamefunguliwa rasmi leo Novemba 25,2025 na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Bw. Peter Juma Lehhet.
Akizungumza wakati wa ufunguzi huo, Bw. Lehhet amesema kuwa mafunzo hayo yameandaliwa kwa lengo la kuwawezesha washiriki kupata uelewa na ujuzi sahihi kuhusu mchakato wa uandaaji wa mpango na bajeti, ili kuboresha upangaji, utekelezaji na usimamizi wa rasilimali za Halmashauri kwa ufanisi, uwazi na uwajibikaji.
Ameongeza kuwa uboreshaji wa uwezo wa watumishi katika eneo la mipango na bajeti ni muhimu kwa kuhakikisha kwamba shughuli na miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa kuzingatia vipaumbele vya Halmashauri na matarajio ya wananchi. Aidha, amewataka washiriki kutumia vizuri mafunzo hayo ili kuongeza tija katika majukumu yao ya kila siku.
Mafunzo haya yanatarajiwa kumalizika kesho yakijikita katika maeneo mbalimbali ikiwemo uchambuzi wa mahitaji, upangaji shirikishi, utumiaji wa mifumo ya Serikali kama PlanRep, pamoja na mbinu za bajeti inayozingatia matokeo.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.