Naibu waziri afurahishwa na Miradi mikubwa inayotekelezwa na Halmashauri ya Jiji la Mwanza
Naibu waziri Ofisi ya Rais –TAMISEMI,Mheshimiwa Joseph George Kakunda amefanya ziara ya kikazi katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza na kutembelea miradi Mikubwa inayotekelezwa na Halmashauri ya Jiji la Mwanza na wadau wengine wa maendeleo yenye thamani zaidi ya Shilingi Bilioni 5 za Kitanzania.
Miradi ya Maendeleo iliyotembelewa ni pamoja na Ujenzi wa Machinjio ya Kisasa yenye thamani ya zaidi ya milioni Miatisa,Ujenzi wa Dampo la Kisasa ambao utagharimu zaidi ya Bilioni Nne.
Akiwa Katika Machinjio ya Kisasa Mheshimiwa Kakunda,amewapongeza wadau wa maendeleo LVEMP pamoja na Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa kutekeleza mradi mkubwa wenye kuzingatia athari za mazingira na utakaotoa fursa kubwa za kiuchumi kwa wakazi wa Mwanza
“Niwashukuru kwa kuwekeza kwenye mradi huu mkubwa wa kisasa ambao utaongeza tija katika uchinjaji wa mifugo na uhifadhi wa mazao ya mifugo’’ alisema Mheshimiwa Kakunda.Sanjari na Machinjio Mheshimiwa Kakunda akiwa katika Dampo la Kisasa Buhongwa, alishuhudia namna wananchi walivyovamia eneo hilo. Hivyo kutokana na uvamizi huo Mheshiiwa Kakunda amewataka wananchi wote walioko kwenye “Buffer zone” kuondoka mara moja maeneo hayo kwa ajili ya ustawi wa afya zao
Pamoja na ziara Mheshimiwa Kakunda alifanya Mkutano na watumishi wa Halmashauri na kuitaka Halmashaurii ya Jiji la Mwanza kuweka mfumo mzuri wa kuhifadhi milima ili kuzuia uvamiaji wa maeneo ya milima ili kuzuia athari za mazingira
Pamoja na hilo, Mheshimiwa Kakunda ameiagiza Halmashauri kuteuwa shule kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalum ili kuwafanya walemavu kupata Elimu
Aidha Mheshimiwa Kakunda amesisitiza watumishi kufanya kazi kwa kuzingatia miiko na maadili ya watumishi wa umma hususani kuvaa mavazi yenye haiba.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.