Naibu meya wa JIji la Mwanza awapongeza wanafunzi wa Shule ya Msingi Nyamagana baada ya matokeo
Mheshimiwa Bhiku Kotcha, Diwani wa Kata ya Nyamagana amefanya tafrija ndogo ya kuwapongeza wanafunzi wa Darasa la saba waliohitimu Shule ya Msingi Nyamagana Mwaka 2018 na Halmashauri ya Jiji la Mwanza kuwa miongoni mwa Halmashauri Kumi zilizofanya vizuri kitaifa.
Wakati wa Tafrija hiyo Mhe Kotecha amepiga marufuku wazazi wa watoto kuchangishwa michango aina yoyote ile kwa sababu Mhe Rais anatoa fedha nyingi kugharamia elimu ili wanafunzi wasome lakini kama kuna michango midogo midogo kama fedha za Mlinzi na Bili za Umeme huwa anatoa ili wanafunzi wasome.
Mhe. Kotecha ameongezea kwa kusema huwa anagaramia Mahafali hizi tangu 2016 kwa sababu anajua wazazi wanazidiana kipato hivyo anaamua kuchukua jukumu hilo ili wapiga kura wake wote waunganishwe kwa tukio kama hili.
Hata hivyo Mhe.Kotecha amewaasa wanafunzi kuendelea kuwa na maadili mema na kutojihusisha na makundi mabaya mitaani maana bado wanasafari ndefu kielimu .
Akimalizia Mhe Kotecha amempongeza Mhe Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya kuwaletea watanzania maendeleo
“Leo tupo wengi hapa kwa sababu ya Elimu bila malipo na Hii imefanywa na Mhe Rais” alisema Mhe Kotecha
Mhe.Kotecha mbali na kugharamia Mahafali za shule zake kwenye kata yake pia amechimba kisima cha Maji, Uwekaji wa Umeme na Kujenga Matundu ya Vyoo zaidi ya Ishirini
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.