Mheshimiwa Naibu meya wa Jiji la Mwanza na Diwani wa kata ya Nyamagana Bhiku Kotecha amepokea msaada wa vifaa mbalimbali vya Hospitali kutoka " Lions Club of Victoria" walioko Jijini Mwanza.
Vifaa vilipokelewa ni pamoja na madawa, jokofu la kuhifadhia madawa, mizani ya kupimia uzito,vifaa vya kupimia kisukari, Kiti cha kusukumia wagonjwa, kifaa cha kupimia presha,
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo gavana wa Lions Club of Mwanza Ndugu Kanji Rizwan amefurahishwa na utendaji kazi wa Mhe shimiwa Kotecha kwa kuwashirikisha wadau mbali mbali wa maendeleo katika kata yake.na kulithamini hilo Bwana Kaji amemtunuku beji ya Lions Club.
Aidha Bwana Kaji amesema taasisi yao hiyo imekuwa mstari wa mbele kuchangia katika sekta ya afya akisisitiza kuwa hata Jana walikuwa hospitali ya Bugando kuwasaidia watoto wenye saratani.Akiongea wakati wa kupokea vifaa hivyo mheshimiwa Kotecha amewashukuru Lions Club kwa mchango wao huo huku akiwaomba wakiguswa tena kusaidia wamsadie kukarabati jengo moja walilopewa na Halmashauri ili waweze kulitumia kama wadi ya akina mama suala ambalo limepokelewa na Lions club kuhaidi kuanza kulikarabati wiki hii
Msaada wa vifaa vilivyotolewa unakadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya Shilingi.milioni mbili za kitanzania.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.