Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo hufanyika kila mwaka Machi 8 yameadhimishwa mkoani Mwanza Leo March 6 , 2025 katika uwanja wa Nyamagana na kuhudhuriwa na viongozi pamoja wanawake kutoka wilaya zote za mkoa wa Mwanza huku mgeni rasmi akiwa ni mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh.Said Mtanda kwa kauli mbiu ya Mwaka huu isemayo " Wanawake na wasichana 2025 ; Tuimarishe Haki , Usawa na Uwezeshaji "
Katika Maadhimisho hayo Mgeni rasmi Mh.Said Mtanda amewataka wanawake wa mkoa wa Mwanza kutathimini mafanikio na changamoto zilizopo katika jitihada za kutoa fursa sawa Kwa wanawake na wanaume kushiriki katika harakati sawa za kuboresha maisha bila ubaguzi wa kijinsia.
"Niwatake wanawake wa mkoa huu kutathimini Mafanikio na Changamoto bila ya ubaguzi " amesema Mh. Said Mtanda.
Aidha , Mh. Said Mtanda ameleza sababu ya uwepo wa siku ya Wanawake Duniani iliyoanza mwaka 1977 huko nchini Marekani ambayo ilikuwa ni siku rasmi juu ya haki za wanawake ambapo walidai kulipwa ujira mkubwa , kupunguziwa muda wa masaa ya kazi pamoja na haki ya kupiga kura.
Vilevile , Mh. Said Mtanda amewashukuru wanawake wa mkoa wa mwanza Kwa zawadi ambazo wamempatia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan na kuhaidi zitamfikia kupitia wasaidizi wake.
Maadhimisho ya Siku ya Wanawake ni Jambo la Msingi Kwa Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Kila Mtu Kwani Wanawake Wanachangia Kwa Kiasi Kikubwa Katika Familia , Jamii na Uchumi wa Taifa .
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.