Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mhe. Amina Makilagi amewapongeza wananchi wa mtaa wa Bugayamba Kata ya Lwanhima kwa kujitoa kwa gharama zao na kuanzisha ujenzi wa misingi minne kwa ajili ya Shule Mpya Bugayamba kabla ya Serikali kutoa fedha na kukamilisha ujenzi huo.
Mhe. Makilagi ametoa pongezi hizo Leo wakati wa ufunguzi wa Shule hiyo ambayo imekuwa msaada mkubwa kwa wakazi wa eneo hilo kutokana na kuwa na Shule Moja ya Sahwa iliyokuwa imelemewa na Idadi kubwa ya wanafunzi.
“Niwapongeze wazazi kwa kuona mbali na kuanza kuchangishana mkanunua kiwanja na kuanzisha ujenzi kwa gharama zenu kweli mliona mbali na Serikali sikivu ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ikamwaga fedha na kumalizia ujenzi huu ambapo Leo wanafunzi zaidi ya 800 wanasoma bila wasiwasi”, amesema Makilagi
Mhe. Makilagi pia ametoa rai kwa wazazi kuendelea kuhimiza masomo kwa watoto na kutokuwa kikwazo cha kukatisha masomo yao kwa kuwapa Majukumu mengine na kuongeza kuwa ikibainika hatua Kali zitachukuliwa kwa wazazi hao.
Aidha amewahimiza wazazi kuhakikisha wanachangia kwa ajili ya chakula cha watoto wao wawapo shuleni kwani kufanya hivyo kunawarahisishia walimu kuwafundisha kwa kuelewa wanachofundishwa tofauti wakiwa na njaa.
Mhe. Makilagi pia ameweza kuchangia magunia matano ya mchele, unga wa lishe, kunde na choroko kwa ajili ya kuhamasisha wazazi kwenye jambo hili.
Kwa upande wake Afisa Elimu Msingi Mussa Lambwe kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza akimwakilisha Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Wakili Kiomoni Kibamba amesema Shule imepatikana Muhimu kulinda miuondombinu na kusoma kwa bidiii.
Katika hatua nyingine Lambwe amewataka wazazi kuwa makini na watoto wao hasa kipindi hiki ambacho Dunia imebadilika na kuwaambia ukweli juu ya sehemu zao za nyeti na nani anatakiwa kuzishika Ili kukomesha vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.