Mhe. Amina Nassoro Mkilagi Mkuu wa wilaya ya Nyamagana leo tarehe 26April, 2024 amewataka Wananchi wa Mtaa wa Majengo - Nyegezi Wilayani Nyamagana kuu enzi na kuuthamini Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ili kuendelea kulinda Amani, upendo na Mshikamano uliopo kwa faida ya kizazi kilichopo na vizazi vijavyo.
Mhe. Makilagi ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Majengo katika Shule Mpya ya Majengo Shule ya Msingi ambapo amewaeleza wananchi kuwa zipo faida nyingi tunazo furahia sasa ambazo kupitia Muungano huu tumezipata ikiwemo maendeleo lukuki yaliyoletwa na Waasisi wetu pamoja na Mama yetu Rais Samia Suluhu Hassan.
Maadhimisho haya Wilayani Nyamagana yameenda sambamba na zoezi la kupanda miti na kufanya usafi, ambapo Wananchi pamoja na Wanafunzi wa eneo la Majengo Kata ya Mkolani wameungana kuadhimisha siku hii muhimu na jumla ya miti elfu moja (1000) imepandwa katika Shule ya Msingi Majengo.
Mhe. Makilagi amewasisitiza Wananchi wote wa eneo la Majengo kuhakikisha wanailinda na kuitunza vema miti yote iliyo pandwa ili iwafae baadaye kwani ni muhimu kwa wanafunzi kwakuwa itawapatia matunda, kivuli na urembo utakao ifanya Shule ya Msingi Majengo kuwa na mazingira ya kuvutia kwa wanafunzi, Walimu na wananchi kwa ujumla.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.