Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mheshimiwa Marry Tesha Onesmo ametoa muda wa Mwezi mmoja kwa wamiliki wa vyombo vya kusafirisha abiria na mizigo kama Boda boda,Bajaji,Taxi, Virikuu(ambao hawajasajiliwa) Kuhakikisha wanasajiliwa ifikapo tarehe 21/04/2018.
Mheshimiwa Tesha ameyasema hayo jana alipofanya Mkutano na waandishi wa Habari ofisini kwake ambapo amesema kwa mujibu wa sheria ndogo ndogo za Halmashauri vyombo hivi vinatakiwa visajiliwe na kulipa Kodi/ushuru ambapo Pikipiki za Miguu mitatu na kirikuu ni shilingi elfu Tano, na Taxi ni shilingi Elfu Kumi Kwa Mwaka.
Sanjari na hilo ,Mheshimiwa Tesha pia amezungumzia utekelezaji wa agizo la waziri Mkuu la kuhakikisha wanafikia wananchi kwenye kata zao tofauti na walivyokuwa wanafanya hapo awali kutenga siku ya Juma nne na kukaa na watalaamu kwenye Ukumbi wa Ghandhall kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi.
“Tumeamua kubadili mfumo wa kusikiliza kero za wananchi kwa sasa tunawafuata wananchi kwenye kata zao,baada ya kushauriwa na waziri Mkuu kuwafikia wananchi na tayari tumeshaanza tangu tarehe 13/03/2018” amesema Mheshimiwa Tesha.
Aidha Mheshimiwa Tesha amesema Ratiba hiyo itaendelea kwenye kata zote 18 na itafikia tamati tarehe25/04/2018
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.