Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda, Amefanya kikao na Waandishi wa Habari leo Julai 22,2024 katika uwanja wa Nyamagana kwa lengo la kufungua rasmi uuzwaji wa Tiketi kuelekea kilele cha Tamasha la Pamba Day tarehe 10 Agost, 2024 katika viwanja vya CCM Kirumba.
Akizungumza katika Uwanja wa Nyamagana amewaeleza wadau wa soka na wapenzi wa Mpira wa Miguu kuwa kuelekea kilele cha Tamasha la Pamba Day katika Uwanja wa Ccm Kirumba tiketi za bei tofauti tofauti zitaanza kuuzwa mapema hivi leo baada tu ya uzinduzi wa tiketi hizo kwa ghrama ya shilingi za Kitanzania 50,000/= V.I.P, 20,000/=, 10,000/= na 3,000 mzunguko ili kila shabiki wa Pamba FC apate fursa ya kushiriki na kuishangilia timu yake pendwa.
Mhe, Said Mtanda ameongeza kuwa siku ya Tamasha la Pamba Day Wachezaji wote watatambulishwa rasmi sambamba na kuutambulisha uongozi wote wa timu yetu pendwa, zoezi litakalo kwenda sambamba na mechi ya kirafiki itakayochezwa uwanjani hapo ambapo burudani mbalimbali kutoka kwa Wasanii wetu wa ndani na nje ya Mwanza watatumbuiza akiwemo FID Q, Harmonize na wengine wengi kutoka kanda ya ziwa na Tanzania kwa ujumla.
Pia Mkuu wa Mkoa ameipongeza Bodi ya Timu ya Pamba kwa kazi waliyoifanya ikiongozwa na Msitahiki Meya wa Jiji Mhe, Sima C. Sima na Mwenyekiti wa Pamba Jiji FC Mhe. Bhiku Kotecha kwa kazi nzuri waliyoifanya ya kuisimamia Timu ya mpira hadi leo ipo kambini kwa ajili ya maandalizi na siku yoyote watarejea kwa ajili ya Tamasha la pamba day.
Mkuu wa Mkoa Mhe, Said Mtanda amemaliza kwa kutoa wito kwa wapenzi na wadau wa mpira kuwa baada ya leo waendelee kukata tiketi katika Ofisi za Mkurugenzi, Ccm kirumba, Nyamagana, Ofisi za kata na Matawi yote ya Timu za Pamba ikiwa ni pamoja na kununua tisheti ili kila shabiki apate Tisheti yake kwa wakati, huku akisisitiza kuepuka matapeli kwa maana tikeki zote zinazotolewa ni za mashine.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.