Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amefanya kikao kazi na watumishi wa umma leo July 15,2024 katika ukumbi mkubwa wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa lengo la kuwakumbusha majukumu na wajibu wao katika kazi.
Mhe. Said Mtanda ambaye pia ni mwenyekiti wa kikao hicho amewakumbusha watumishi mambo ya kuzingatia katika kazi ikiwa ni pamoja na Nidhamu katika kazi, Mawasiliano na Mahusiano, Mapato na matumizi na kusema kati ya asilimia kumi Halmashauri wameshatoa 8% na wamalizie hizo 2% zilizobaki ili ziende kwenye miradi ya maendeleo. Lakini pia amesisitiza kuwahudumia wananchi kwa upendo mkubwa hasa kwa kuwa wabunifu ikiwa ni pamoja na kuboresha maeneo ya mapokezi.
Ameendelea kuwaeleza watumishi kuwa Mkoa wa Mwanza umepatiwa kiasi cha shilingi bilioni 37 na Serikali kwa ajili ya miradi ya maendeleo, hivyo atahakikisha fedha hizo zinatumika kikamilifu kwa kutekeleza miradi ya serikali ili kupunguza changamoto zilizopo katika Wilaya ya Nyamagana.
Vilevile, Mhe. Said Mtanda akitolea ufafanuzi changamoto atakazozitatua katika Wilaya ya Nyamagana, ni pamoja na maji licha ya kuwa na mradi wa maji Butimba uliogharimu zaidi ya Bilioni 79 ameahidi ataongeza mtandao wa maji kwenye maeneo yenye changamoto, pia kuweka mafuta kwenye magreda yatakayotumika kuchonga barabara, na kwa upande wa madarasa amesema ataweka namna nzuri ya wananchi washiriki kikamilifu katika ujenzi ili kuweka mazingira rafiki kwa wanafunzi kujisomea.
Kupitia kikao hicho Mhe. Said Mtanda amewaeleza watumishi na wananchi kupitia vyombo vya habari vilivyoudhuria kuwa timu ya Pamba Jiji Fc ni mali ya wananchi wa Mwanza hivyo hawana budi kuiunga mkono, na kuuasa uongozi mpya wa Pamba Jiji kusimamia msimamo wa timu na wasiyumbiswe na watu wa mtaani. Pia alitumia fursa hiyo kuwashukuru wadhamini waliyojitokeza kuidhamini timu ya Pamba Jiji Fc ikiwa ni pamoja na GSM, Primier-bet, na Jambo. Pia amesisitiza matarajio ni kwamba wanahitaji ifikie mahali Timu ya Pamba ijiendeshe yenyewe bila kutumia fedha za umma.
Mwisho, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ameipongeza Halmashauri kwa kuendelea kuwa na hati safi licha ya kuwa na hoja 97 na kubaki 17 ambazo zote zimejibiwa, na kuongeza kuwa mapato ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza yamepanda, hivyo basi Mkurugenzi asichoke aendelee na kasi hiyohiyo ya ukusanyaji mapato.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.