Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Wakili Kiomoni Kiburwa Kibamba amefanya mazungumzo na waandishi wa habari leo Mei 2, 2024 katika ofisi yake, kwa lengo la kupaza sauti kwa wananchi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza kuwaomba na kuwasihi kulipa ushuru, kodi na ada mbalimbali kwa hiari bila shuruti.
Wakili Kibamba amesema kwamba, Kabla ya tamko hili Halmashauri ilifanya juhudi mbalimbali kuwakumbusha wananchi kulipa kodi kupitia watendaji wa mitaa na gari la matangazo lakini walio wengi bado hawajalipa kodi zao na tumebaki na miezi miwili tu mwaka wa fedha kuisha hivyo basi ndani ya hiyo miezi tumejipanga kukusanya kodi pasipo kupoteza hata senti moja. Hivyo nawaagiza wahusika kulipa mara moja kuepuka usumbufu.
Aidha Wakili Kibamba ameongeza kuwa kwa upande wa leseni za Biashara zilizosajiliwa ni 16091 na maombi yaliyoidhinishwa kwenye mfumo ni 15591 na ambayo hayakuidhinishwa ni 43 kati ya hizo leseni ambazo zimetolewa ni 12209 sambamba na hivyo kuna wafanya biashara 3310 ambao hawajalipa leseni pamoja na ushuru wa huduma 3600, 72000 na 108000 na wafanya biashara 685 wana control namba lakini bado hawataki kulipa. nawasihi walipe kabla hatujawafungia maduka au kuwapeleka mahakamani kwa mujibu wa sheria.
Vilevile amesema kwenye maegesho ya magari zipo kampuni 86 ambazo wana maegesho maalum, amewataka kuonesha lisiti maalum za malipo, na wasiolipa walipe na kuongeza kuwa maegesho yote yatavunjwa na kupangwa upya kwa kupitia mikataba yao na pia wachukue control namba walipe.
Nao wamiliki wa vizimba na vyumba kwenye masoko wanasisitizwa kulipa kodi ya pango wasisubiri kufungiwa au kupelekwa kwenye Mahakama inayotembea sambamba na waliojenga bila vibali wajisalimishe kulipa faini kwa mujibu wa sheria.
Mwisho amemaliza kwa kusisitiza kuwa ulipaji kodi unafanywa kupitia control namba, na wale wenye POS ndo wanaoruhusiwa kukusanya ushuru kwa sababu wanatoa lisiti, malipo yatakayo fanyika kinyume na hivyo Halmashauri haitahusika.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.