Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza Wakili Kiomoni Kibamba amekutana na wafanyakazi wa Halmashauri katika kikao maalum cha tathmini ya ukusanyaji wa mapato kilichofanyika Desemba 29, 2025 katika ukumbi mkubwa.
Kikao hicho kimefanyika leo Desemba 29, 2025 katika ukumbi mkubwa wa Jiji kikiwa na lengo la kupima utekelezaji wa majukumu ya ukusanyaji wa mapato katika Idara na vitengo mbalimbali pamoja na kubaini changamoto zilizojitokeza.
Katika kikao hicho, wasimamizi wa vyanzo vya mapato waliwasilisha taarifa zao, lakini Mkurugenzi hakuridhishwa na kiwango cha mapato kilichokusanywa. Kutokana na hali hiyo, alitoa maelekezo na msisitizo mkali akisisitiza uwajibikaji, uaminifu na ufanisi kwa watumishi wote wanaohusika na ukusanyaji wa mapato.
Akiangazia Stendi ya Mabasi ya Nyegezi, Mkurugenzi aliagiza kuondolewa kwa wakusanyaji wa mapato wasio waaminifu na nafasi zao kujazwa na watu wenye uadilifu na weledi. Vilevile, aliwahimiza wasimamizi wa vyanzo vingine vya mapato kuhakikisha kila shilingi inayostahili kukusanywa inakusanywa ipasavyo.
Aidha, Mkurugenzi alisisitiza kuendelea kutumia mfumo wa ukusanyaji wa mapato wa Balozi System, ambao utaanza kufanya kazi kuanzia ngazi ya mtaa hadi kata. Hatua hii inatarajiwa kuongeza uwazi, uwajibikaji na ufanisi katika ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Hatua hizi zinatarajiwa kuongeza uwazi, uwajibikaji na ufanisi katika ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza, hivyo kuchangia katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na utoaji wa huduma bora kwa wananchi.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.