Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza wakili Kiomoni K. Kibamba amefanya ziara na kikao cha tathimini ya hatua zilizofikiwa katika upembuzi yakinifu wa Mpango kabambe wa usafiri wa umma wa Jiji la Mwanza ( Master Plan for Urban Transport System and Bus Rapid Transit System Development in Mwanza City).
Mpango Kabambe wa Usafiri wa Umma unaandaliwa na kampuni za ushauri za DOHWA, YOOSHIN ENGINEERING na TRACOM CONSORTIUM kutoka Korea chini ya ufadhili wa Serikali ya Korea Kusini na International Contractors Association of Korea ( ICAK).
Aidha Wataalam washauri waliwasilisha ripoti na kueleza kuwa shughuli inaendelea vizuri na itakamilika Juni 2026.
Mpango kabambe wa usafiri wa umma na mabasi ya mwendokasi una lengo la kutatua changamoto za ukuaji wa Majiji katika sekta ya usafirishaji wa umma kwa kuondoa msongamano wa magari, abiria, kudhibiti ajali za barabarani, uchafuzi wa hewa na mazingira, kuhakikisha usalama wa wananchi kwa kutumia miundombinu rafiki ya usafirishaji, kuwezesha wananchi kufikia huduma mbalimbali za Jamii kwa wakati, kuongeza tija ya uwajibikaji, kuzalisha fursa za ajira kutokana na uwekezaji katika kuboresha miundombinu ili kuwa na maendeleo endelevu ya Jiji la Mwanza.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.