Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mhe.Dkt Philis Nyambi amesema miradi itakayotembelewa na Mwenge wa Uhuru 2018, inajumuisha Ujenzi wa Zahanati ya Isebanda, Soko la Igogo,Milioni 200 mikopo ya wanawake ,Vijana na walemavu na ujenzi wa Shule ya Msingi Buhongwa B
“Pamoja na miradi mingine mikubwa tunayotekeleza naahidi kutoa milioni 200 kwa vikundi vya biashara vya wanawake,vijana na walemavu ambapo fedha hiyo inatoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza” amesma Dkt Nyimbi
Akizungumza wakati wa ziara hiyo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella amesema kwa Tsh milioni 200 watakazokopeshwa wafanyabiashara ndongo ndogo (machinga) itaongeza tija kwenye biashara zao na kuwanyanyua kiuchumi.
Aidha Mkuu wa Mkoa amewapongeza wamachinga kwa kuendelea kuleta amani,,utulivu na mshikamano kwenye Jiji la Mwanza.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa amesisitiza suala la usafi kuendelea kuwa tamaduni za kila siku kwa wafanyabiashara ndogondogo ili kuepuka magonjwa ya malipuko.
Mhe.Mongella amesisitiza kuwa Mheshimiwa Rais anataka wachapa kazi, na mkopo huo utawalenga wanaofanya kazi kwa bidii ili waweze kuzalisha na kuweza kurejesha mkopo kwa ajili ya vikundi vingine kufaidi
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.