Shule ya Sekondari Mtoni imechangisha zaidi ya milioni Kumi kwenye maadhimisho ya miaka 10 ya shule hiyo ya sekondari ambayo yalifanyika katika kata ya Mabatini jijini Mwanza.
Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na Mheshimiwa Mary Tesha Onesmo (Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana ) Ambaye alimuwakilisha Mgeni Rasmi wa siku hiyo Mheshimiwa John Mongela Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ambaye hakufika kwa kutingwa na majukumu mengine ya Kitaifa.
Maadhimisho haya yalizinduliwa kwa Shule na Jamii husika kufanya usafi wa mazingira katika kata ya Mabatini, Mgeni rasmi kupanda miti katika eneo la shule,maonesho mbalimbali ya Wanafunzi, Vikundi vya ngoma za asili na kwaya ya shule kutumbuiza .
Akitoa Salamu zake Mheshimiwa Mary Tesha Onesmo alifurahishwa kwa Uongozi mzuri aliouonyesha Mheshimiwa Diwani wa Kata ya Mabatini “ Pamoja na tofauti za itikadi za vyama vya siasa Mheshimiwa Diwani ameweka mbele suala la maendeleo na leo anatekeleza ilani ya chama Tawala, ni vyema viongozi wengine tukaiga hili” Mheshimiwa Mary Tesha
Aidha Mgeni rasmi alimtaka Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza kutoa fidia kwa Mzee mwenye soko la samaki eneo hilo la shule, ili aweze kuondoka ili shule iwe na eneo la kutosha la kujenga ofisi.
Bi Mary Tesha Onesmo pia aliipongeza shule pamoja na Bodi yake kwa kuwa wabunifu na kuona ni vyema katika maadhimisho hayo kufanya changizo kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Shule na Maktaba.
Akiongea wakati wa maadhimisho hayo Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Ngd Omary Kamata aliupongeza Uongozi wa Shule na Kamati ya Maendeleo ya Kata ya Mabatini kwa Jitihada wanazozifanya za kuwashirikisha wananchi kwenye suala zima la maendeleo ya shule.
Aidha Kaimu Mkurugenzi aliahidi kuwa Baada ya Shule kumaliza kujenga Boma la Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Shule na Maktaba alimashauri itapaua jengo hilo.
Lengo la Changizo ni kupata kiasi cha Milioni Hamsini kwa lengo la kujenga ofisi ya Mkuu wa Shule na Maktaba ya Shule,Lakini Harambee ilichangisha kiasi cha zaidi milioni kumi ikiwa Milioni Mbili imetolewa na wananchi,Milioni Moja ilipatikana siku hiyo na Ahadi ya zaidi ya Shilingi Milioni Nane za Kitanzania.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.