Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mheshimiwa John Mongella leo ameongoza zoezi la ugawaji vitabu katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Zoezi hilo limefanyika leo katika shule ya Msingi Buhongwa.
Akiongea wakati wa zoezi hilo Mhe. Mongella amesema Mkoa wa Mwanza umepokea vitabu 500,466 vyenye thamani ya Bilioni 1.3 Kutoka kwa Mhe.Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John P.Magufuli kwa ajili ya wanafunzi wa Darasa la I,II na III vitabu hivi vinajumuisha vitabu vya Michezo,Kusoma, Afya na mazingira na kuandika. Katika Idadi hiyo Halmashauri ya jiji la Mwanza inapata Jumla ya Vitabu 60705 vya kiada.
Aidha Mheshimiwa Mongella amesema pamoja na Jitihada kubwa zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano ya kuboresha na kutoa elimu bila malipo kwa watanzania ,watanzania wameitikia wito wa kuwapeleka watoto shule na kufanya miundo mbinu ya baadhi ya shule kuzidiwa .Hivyo ni vyema wazazi wakashirikishwa kuchangia kwa ajili ya kutatua matatizo madogo madogo kama vile Matundu ya vyoo “serikali ni wananchi na sisi viongozi ni vielelezo tu hivyo si vyema wananchi kuona masuala ya maendeleo hayawahusu yanahusu serikali” amesema Mhe.Mongella
Mkuu wa Mkoa ameendelea kusisitiza walimu kutekeleza majukumu yao ya kufundisha kwa bidii na kuwawajibisha wanafunzi wenye utomvu wa nidhamu kwa mujibu wa sheria na taratibu ili kujenga nidhamu kwa wanafunzi.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo Mstahiki meya wa Jiji la Mwanza Mhe.James Bwire amewataka walimu kuvitunza vitabu hivyo na kuhakikisha wanafunzi wanavisoma kwa ajili ya kupata maarifa.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya zoezi hilo Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Kiomoni Kibamba Kiburwa amemshukuru Mhe.Rais kwa jitihada kubwa anazozifanya katika kuimarisha na kuboresha Elimu.
Aidha Kibamba amesema amesema kwa sasa wamepokea vitabu 60700, na mwaka Jana walipokea vitabu 71,000 hali inayopelekea shule za msingi kuwa na uwiano wa Mtoto Mmoja Kitabu Kimoja
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.