Ikiwa ni january 09-2024 Mkuu wa Mkoa, Kamati ya siasa na wataalam kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza wametembelea Shule ya Msingi Kanenwa iliyopo kata ya Kishiri na shule ya sekondari Mirongo iliyopo kata ya Mbugani nakutoa nasaha zao kama viongozi.
Mheshimiwa CPA Amos Makala amepokea taarifa ya shule ya Msingi Kanenwa iliyojengwa kwa mradi wa Boost uliogharimu kiasi cha Tsh million 540 ikiwa na jumla ya Madarasa 16 ambayo 14 ni ya Elimu msingi na 2 ni kwa ajili ya watoto wa awali na matundu ya vyoo 27 na jumla ya wanafunzi 250 wamesajiliwa na wengine 654 wamehamia kutoka Bukaga shule ya msingi, suala ambalo limesaidia kuepusha usumbufu kwa wanafunzi waliyokuwa wakitembea umbali mrefu kufata huduma ya Elimu.
CPA Amos Makala mkuu wa mkoa wa mwanza amesema "Shule zote za Mwanza zimesajiliwa kwa mujibu wa sheria" hivyo anatoa pongezi kwa wazazi kwa mchango waliyoutoa katika ujenzi wa shule ya Kanenwa na kwa jitihada zao za kuwaleta watoto kusoma anawahimiza waendelee kutilia mkazo suala la elimu kwani ni haki ya mtoto kusoma.
Vilevile Mkuu wa Mkoa ameuagiza uongozi wa Halmashari ya jiji kuhakikisha maji na umeme vinafika kwa wakati ili kukidhi miundombinu ya shule kwa kuwafanya wanafunzi kuwa na mazingira rafiki ya kujisomea.
Mkuu wa mkoa wa mwanza amekagua ujenzi wa madarasa kwa mfumo wa Ghorofa katika shule ya Sekondari Mirongo iliyopo kata ya Mbugani yenye "wanafunzi 1264 na wanafunzi waliochaguliwa kulipoti hapo ni 223 ikiwa wavulana ni106 na wasichana ni 117 hivyo tu baada ya idadi hiyo kukamilika wanafunzi watafundiswa kozi ya awali ya kingereza kwa majuma 6"kama utaratibu ulivyowekwa na shule hiyo lipoti hiyo imetolewa na miss Masenya mkuu wa shule.
Vilevile Mbunge Mhe Stansilaus Mabula na Katibu wa chama cha mapinduzi Ndg, Robert Karega wameishukuru serikali kwa kuendelea kutekeleza IIani ya chama cha mapinduzi kwa ujenzi wa madarasa, pia wamewashukuru wananchi kwa kuendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali ili kuhakikisha watoto wanapata haki yao ya elimu pasipo kipingamizi.
Waalimu wametakiwa kuhakikisha wanafunzi wanaripoti shule kwa wakati na kutambua idadi ya wanafunzi ambao hawatafika na sababu zinazowafanya wasifike shule kabisa na kutoa taarifa kwenye ofisi zao za kata kwa uchunguzi zaidi kwani kila mtanzania anayo haki ya kupata elimu.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.